Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Tumtazame mwanamke kama injini ya maendeleo

Дата публикации: 09-08-2026 08:18:51

​Mapema asubuhi, kabla hata jua halijachomoza na kuangazia paa za bati za sokoni, sauti ya mama Asha inasikika ikivuma kwa uchangamfu.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumapili, Agosti 09, 2026

​Mapema asubuhi, kabla hata jua halijachomoza na kuangazia paa za bati za sokoni, sauti ya mama Asha inasikika ikivuma kwa uchangamfu. 

Akiwa amepanga vizuri mafungu ya nyanya, vitunguu, na miche ya mboga mboga juu ya meza yake ndogo ya mbao, yeye ndiye kiini cha uhai wa soko hili.

Mama Asha ndiye mfadhili mkuu wa masomo ya watoto wake watatu wanaosoma shuleni na vyuoni. Kupitia biashara hii ndogo, amekuwa nguzo inayotegemewa na wakulima wa vijijini wanaomletea bidhaa, na walaji wa mjini wanaotafuta lishe bora.

​Mita chache kutoka soko hilo, katika hospitali ya wilaya, Daktari Grace anasimamia wodi ya wazazi akiwa na utulivu mkubwa. 

Mikono yake, ambayo miaka 20 iliyopita ilikuwa ikibeba kuni huko kijijini, sasa inaokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga kila uchao. Usiku wa leo, ameshinda chumba cha upasuaji akipambana na vifo vitokanavyo na uzazi, akihakikisha kuwa nguvu kazi ya kesho inazaliwa salama na salama.

Hivi ni visa vya kutunga, lakini vyenye mafundisho makubwa na vinavyoakisi uhalisia katika jamii zetu. Mama Asha sokoni na Dk Grace hospitalini, ni mifano hai ya ukweli mmoja usiopingika: mwanamke si mtazamaji wa maendeleo, bali ndiye injini kuu inayosukuma mbele gurudumu la jamii hasa kama kuna mazingira yaliyojengwa kumfanya awe hivyo 

​Kisa hiki cha wanawake hawa wawili kinadhihirisha nguvu kubwa iliyojificha ndani ya mwanamke pale anapopewa nafasi na kuaminiwa. 

Maendeleo ya jamii yoyote ile hayawezi kukamilika ikiwa nusu ya nguvu kazi yake ambayo ni wanawake, itaachwa nyuma au kuonekana kama viumbe wa daraja la chini.

 Wakati umefika wa kutambua kuwa mwanamke akiwezeshwa kwa kujengewa mazingira rafiki ya kisheria, kijamii, na kiuchumi, anakuwa na uwezo wa kuleta mageuzi makubwa yanayovuka mipaka ya familia yake na kugusa taifa zima.

​Uwezeshaji wa kiuchumi kwa mwanamke huanza na kuondolewa kwa vikwazo vya kimfumo na kitamaduni vinavyombagua.

Katika jamii nyingi, mwanamke amekuwa akikabiliwa na ukuta mnene wa kutomiliki rasilimali kubwa kama ardhi, au kukosa fursa za kiuchumi kwa sababu ya kutofikiriwa kama mfanya uamuzi wa kifedha.

 Hata hivyo, tafiti na mifano ya kiuhalisia inaonyesha kuwa, mwanamke anapowezeshwa kumiliki ardhi na kupata mitaji, matokeo yake huwa na tija kubwa zaidi.

​Mwanamke hawekezi faida yake kwenye anasa; anawekeza kwenye lishe bora ya familia, afya, na elimu ya watoto wake.

Hili linapofanyika, jamii inaondokana na mzigo wa magonjwa  na inatengeneza kizazi kijacho chenye akili na nguvu ya kufanya kazi. 

Kujenga mazingira yasiyobagua, kama vile kuweka sera rafiki za kodi kwa wajasiriamali wadogo wa kike na kuwapa elimu ya kifedha, kunamtoa mwanamke kutoka kwenye uchumi wa kijikimu na kumuingiza kwenye uchumi wa ushindani na uzalishaji mkubwa.

​Zaidi ya sekta ya kiuchumi, ushahidi wa mwanamke kuwa injini ya maendeleo unaonekana wazi pale anaposhika hatamu za uongozi katika sekta za elimu na siasa. 

Katika miaka ya hivi karibuni, tumeshuhudia wanawake wakiaminiwa na kushika nafasi za juu kabisa za uamuzi kuanzia ngazi za vijiji, uongozi wa vyuo vikuu, wizara, hadi urais wa nchi.Mfano mzuri ni nchi kama Namibia na Tanzania zenye marais wanawake.

Kupitia uongozi, wanawake wameonyesha sifa za kipekee za umakini, kupinga rushwa, na kuweka msisitizo kwenye masuala yanayogusa maisha ya kila siku ya mwananchi, kama vile upatikanaji wa maji safi na kuboresha miundombinu ya shule. Katika sekta ya elimu, mapinduzi makubwa yanafanyika pale wasichana wanapowezeshwa kusoma masomo ya sayansi na teknolojia.

Hawa wanakuja kuwa wavumbuzi na maprofesa wanaotatua changamoto za kijamii kwa kutumia weledi wao. 

Kila mwanamke anayeshika hatamu leo, anasimama juu ya mabega ya mfumo uliomwamini na kumpa uwezeshaji stahiki.

​Ni makosa makubwa kumtafuta mwanamke katika muktadha wa majukumu ya nyumbani pekee. Ingawa kulea na kuwa mama ni jukumu la heshima kubwa, mwanamke akiwezeshwa anaonyesha kuwa yeye ni zaidi ya mama; yeye ni kiongozi wa kiroho, mwanadiplomasia, mwanasayansi, na mhimili wa amani.

​Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kusuluhisha migogoro ya kijamii na kulinda amani kutokana na asili yao ya kuwa na diplomasia na huruma. Wanaposhirikishwa kikamilifu, wanakuwa sauti ya wanyonge na watetezi wa haki za kibinadamu.

 Mchango wao katika sekta zisizo rasmi na zile rasmi unachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa (GDP), huku wakijenga mifumo ya kijamii inayojali utu na usawa.

​Mwanamke si kiumbe wa daraja la chini anayepaswa kusubiri hisani, bali ni nguvu kazi thabiti inayohitaji mazingira wezeshi ili itoe matunda yake kwa ukamilifu.

Jamii yoyote inayotaka kupiga hatua za haraka za kimaendeleo haina budi kuweka nguvu zake katika kumtengeneza mwanamke kuanzia mtoto wa kike shuleni hadi mjasiriamali wa sokoni. 

Hapo tutakuwa sio tu tumemwezesha, lakini tumemuongezeea majukumu kuwa yeye ni zaidi ya mama. Anaweza kufanya makubwa ya kimaendeleo kwa jamii yake zaidi ya kuwa mtunza watoto nyumbani. 

Abeid Poyo ni mhariri wa makala wa Mwananchi.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune01009-08-2026
2Sendiga ‘anavyowateka’ wananchi kwa kujifananisha nao01028-07-2026
3Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
4Usalama wa kihisia msingi muhimu utekelezaji wa mtalaa05.5610-08-2026
5Komenti hasi mitandaoni zinavyogeuka shubiri kwa watumiaji09.3212-08-2026
6TUONGEE KIUME: Ujumbe wenu huu hapa mnaojiita wanaume09.3209-08-2026
7KONA YA MALOTO: Kumwelewa Nchimbi inatakiwa ung’amue alikoficha nukta01028-07-2026
8Putzu parea igel jauzkaria laguntzeko0105-06-2026
922 июня в Аше зажгут свечи в память о героях0217-06-2026
10Проект «Ты важна, ты достойна» приветствует новых жителей Ашинского округа и их мам5312-06-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.57. Источник: www.mwananchi.co.tz.