“Niliwahi kuposti video yangu TikTok ghafla watu wakaanza kunishambulia kwa maneno yasiyokuwa mazuri yalinifanya nifute post ile na kujiondoa kwenye huo mtandao.”
Jumatano, Agosti 12, 2026
Dar es Salaam. “Niliwahi kuposti video yangu TikTok ghafla watu wakaanza kunishambulia kwa maneno yasiyokuwa mazuri yalinifanya nifute post ile na kujiondoa kwenye huo mtandao.”
Hayo ni maneno ya mtumiaji wa TikTok ambaye hakupenda jina lake litajwe ambapo anasema maoni yale yalimfanya ajisikie mnyonge, asiye na thamani na pia akihisi kuonewa.
“Kwenye ile video nilikuwa nacheza muziki lakini komenti za watu zilikuwa ni kunishambulia huku wengine wakinitukana matusi mazito,” kwa kweli niliumia,” amesema mtumiaji huyo kutoka Dar es Salaam.
Ushuhuda wa mtumiaji huyo wa mtandao wa kijamii unadhihirisha hofu inayotokana na uwepo wa vitendo vya unyanyasaji maarufu kama ‘cyberbullying’ mitandaoni sehemu ambayo imekuwa muhimu ya mawasiliano hasa vijana.
Ikumbukwe, Cyberbullying ni unyanyasaji au uonevu unaofanywa kupitia teknolojia na mitandao ya kidijitali, kama vile WhatsApp, Facebook, Instagram, TikTok, X, SMS au michezo ya mtandaoni.
Mifano yake ni kama; kumtukana au kumdhalilisha mtu mtandaoni, kusambaza picha au video zake kwa lengo la kumuaibisha, kumtishia au kumfuatilia kwa ujumbe wa vitisho, kusambaza uongo au taarifa za kumchafua mtu, kutengeneza akaunti bandia kwa kutumia jina/picha ya mtu ili kumdhihaki au kumharibia sifa.
Unyanyasaji wa mtandaoni unaweza kusababisha madhara kwa mtendewa hasa kisaikolojia ikiwemo kujichukia, kupata hasira, kujitenga na kutojiona mkamilifu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Zuhura Othman, maarufu Zuchu aliwahi kutoa malalamiko kuhusiana na unyanyasaji anaofanyiwa mtandaoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la The Citizen ya mwaka 2025, Zuchu alizungumza kuhusu kile alichodai unyanyasaji (bullying) na usumbufu (harassment) aliokuwa akikumbana nao.
Zuchu alisema hali hiyo ilikuwa ikimuathiri katika maisha yake binafsi, afya yake ya akili na hata namna anavyotekeleza shughuli zake za kisanii. Kupitia Instagram, alieleza kuwa licha ya mafanikio aliyoyapata akiwa chini ya WCB Wasafi, bado alikuwa akikumbana na bullying na harassment kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.
Tukio hilo linaonyesha namna cyberbullying na unyanyasaji wa mtandaoni unavyoweza kuwaathiri hata watu maarufu, huku mijadala kuhusu maisha yao binafsi ikigeuka kuwa mashambulizi yanayoweza kuathiri ustawi wao na kazi zao.
Mwimbaji na mwigizaji wa Marekani, Selena Gomez, aliwahi kueleza namna unyanyasaji mtandaoni unavyomuumiza kihisia, akisema baadhi ya watu huandika maneno yanayolenga kugusa moja kwa moja udhaifu wa mtu.
Gomez alisema amekuwa akikumbana na changamoto hiyo kupitia mitandao ya kijamii, hasa Instagram, hali inayomfanya wakati mwingine kufuta programu hiyo kwenye simu yake.
“Unapokea maoni ambayo hayakusemi tu kuwa wewe ni mbaya, bali yanaonekana kulenga moja kwa moja nafsi yako,” alisema Gomez katika mahojiano na The New York Times mwaka 2017.
Alisema watu wanaweza kutumia mitandao kuandika kuhusu mapungufu na hali ya kutojiamini ambayo mtu tayari anayo, jambo linaloweza kuongeza maumivu ya kihisia.
Pia, msanii Ed Sheeran amewahi kueleza namna maoni hasi kwenye mitandao ya kijamii yalivyomuathiri, hasa baada ya kuwa maarufu.
Mwimbaji huyo amesema kukabiliwa mara kwa mara na ukosoaji mtandaoni kulimfanya wakati mwingine kuchukua mapumziko kwenye mitandao ili kulinda ustawi wake wa akili.
Ariana Grande pia amekuwa akikabiliwa na maoni makali kuhusu mwonekano wake, mwili na maisha yake binafsi.
Mwimbaji huyo amewahi kuzungumzia namna maoni ya watu kwenye mitandao yanavyoweza kumuumiza mtu, akiwataka watumiaji kuwa waangalifu wanapotoa maoni kuhusu miili na mwonekano wa wengine.
Mwimbaji Billie Eilish naye amezungumzia changamoto za kukabiliwa na ukosoaji na maoni hasi mtandaoni, hasa kuhusu mwili na mavazi yake. Umaarufu wake ulimfanya maisha yake binafsi na mwonekano wake kuwa mada ya majadiliano makubwa kwenye mitandao, jambo alilosema linaweza kuathiri namna mtu anavyojitazama.
Visa vya wasanii hao vinaonyesha namna unyanyasaji mtandaoni (cyberbullying) unavyoweza kumuathiri mtu kihisia, hata pale anapokuwa maarufu na mwenye mamilioni ya wafuasi.
Mtoto Amanda Todd alikuwa na umri wa miaka 15 alipofariki mwaka 2012 baada ya kupitia miaka ya unyanyasaji shuleni na mtandaoni. Alikuwa akinyanyaswa baada ya picha yake binafsi kusambazwa mtandaoni na mtu aliyekuwa akimtishia.
Kabla ya kifo chake, Amanda alichapisha video YouTube akitumia karatasi zenye maandishi kueleza alichokuwa akipitia, ikiwamo bullying, kujidhuru na mawazo ya kujiua. Kisa chake kilizua mjadala mkubwa duniani kuhusu cyberbullying, usalama wa watoto mtandaoni na afya ya akili.
Utafiti uliofanywa na Pew Research Center nchini Marekani kwa vijana 1,316 wenye umri wa miaka 13 hadi 17 umeonyesha asilimia 46 wamewahi kukumbana na angalau aina moja ya unyanyasaji mtandaoni.
Utafiti huo uliofanyika mwaka 2022 ulibaini miongoni mwa vitendo vilivyoripotiwa ni kutukanwa au kuitwa majina mabaya mtandaoni, kusambaziwa uvumi wa uongo na kutumiwa maudhui ambayo hawakuomba.
Hata hivyo, kadiri matumizi ya mitandao yanavyoongezeka, vijana wamekuwa miongoni mwa makundi yanayotumia muda mwingi katika majukwaa ya kijamii.
Changamoto kubwa ni kwamba ujumbe au picha inayosambazwa mtandaoni unaweza kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi, na kufanya madhara ya unyanyasaji huo kuwa makubwa zaidi kuliko mazingira ya kawaida.
Tofauti na unyanyasaji wa ana kwa ana, maudhui yaliyowekwa mtandaoni yanaweza kusambazwa tena na tena, jambo linaloweza kufanya tatizo kuendelea hata baada ya tukio la awali.
Athari za kisaikolojia
Akizungumza na Mwananchi, Mwanasaikolojia Barnabas Nkinga anasema athari ya kwanza kisaikolojia ni kuathirika kwa utu au thamani ya muhusika pale anapodhalilishwa.
‘Kama kudhalilishwa huko kunahusu kazi basi itasababisha kupungua kujiamini kikazi na kama inahusu mwonekano binafsi hali hiyo itaanza kujiona hauna thamani.” amesema.
Akieleza zaidi anasema pia inamfanya mtu asiwe na uhuru wa kufanya jambo ambapo wakati mwingine anaweza kuchukua uamuzi usio sahihi kama vile kujidhuru au kujiua.
“Unapoathirika afya ya akili unaweza kupata changamoto ya kujidhuru, kujiua ama kujitenga, kupata sonona, magonjwa ya akili, mabadiliko ya tabia na kihisia” amesema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | TikTok пен YouTube елдегі заңнама талаптарын сақтауға міндетті | 0 | 2.5 | 30-07-2026 |
| 2 | В работе TikTok произошел сбой | 0 | 0 | 09-07-2020 |
| 3 | TikTok ограничит публикации с преждевременными заявлениями о победителе выборов в США | 0 | 0 | 28-10-2020 |
| 4 | TikTok удалил более 380 тыс. видео в США за нарушение правил соцсети | 0 | 0 | 20-08-2020 |
| 5 | В работе TikTok произошел сбой | 0 | 0 | 12-05-2021 |
| 6 | TikTok запустит новые инструменты для защиты пользователей от буллинга | 0 | 0 | 10-03-2021 |
| 7 | В TikTok прокомментировали указ Трампа о мерах против компании | 0 | 0 | 07-08-2020 |
| 8 | TikTok сделает аккаунты подростков от 13 до 15 лет приватными | 0 | 0 | 13-01-2021 |
| 9 | TikTok запустил функцию родительского контроля | 0 | 0 | 16-04-2020 |
| 10 | TUONGEE KIUME: Ujumbe wenu huu hapa mnaojiita wanaume | 0 | 9.32 | 09-08-2026 |