Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune

Дата публикации: 09-08-2026 08:07:54

Soma zaidi...

Основное содержимое страницы с новостью.

Prime

Jumapili, Agosti 09, 2026

Muktasari:
  • Ndoa yenu si ya malaika wala mataahira wasiojitambua bali binadamu wenye akili na tabia tofauti.

Canada. Katika maisha yetu ya ndoa tuligundua kuwa hakuna kitu kinaua ndoa,  kama ukimya hasa wawili mnapokosana na kukaa kimya au kuepukana bila kuwa tayari kulikabili tatizo. Badala ya kuambiana makosa na ukweli, wengi, hununiana kiasi cha kila mmoja kukaa kimya na kuumia kivyake. Hii, licha ya kusababisha kukua kwa tatizo, husababisha hata magonjwa ya akili hata mwili.

Kuna kisa cha Ajak na Anyuak tulichosimuliwa. Kisa hiki kinahusisha wanandoa wawili waliokosana na kukwepa kutatua matatizo yao kiasi cha mmoja kuishia kujuta na mwingine akiteketea huku kila mmoja akitamani angesema badala ya kujikalia kimya.

Kama binadamu na wanandoa wowote, wawili hawa walikosana sehemu katika maisha yao ya ndoa. Kwanza, baada ya kuoana, waligundua kuwa wana tabia tofauti kinzani.

Mmoja alikuwa muwazi na msemaji ilhali mwingine alikuwa mkimya na mwenye kuficha hisia zake. Hali hizi, licha ya kusababisha msuguano kitabia, ilisababisha kila mmoja kuanza kujifungia kwenye miili yao na kuteseka kimya bila kukabiliana na matatizo waliyosababishiana.

Pili, baada ya wawili kukosana, walianza kununiana na kutowasiliana wakiamini tatizo lingejiishia. Lakini tatizo halikuisha bali kuzidi kuwa kubwa. Baada ya hapo, walianza kuepukana au tuseme kukwepana. Mwishowe, walitengana ndani ya nyumba yao na kuanza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.

Katika ndoa, hii ni hatua na adhabu ya mwisho kwa wawili waliozoea kuwa kitu kimoja. Kutengana kimwili pia husababisha kutengana kiakili kiasi cha kila mmoja kumuona mwenzie kama mgeni na hata adui. Hivi kuna haja kufikia hatua hii hatarishi? Tutajibu baadae.

Tatu, baada ya tatizo kuzidi kukua na mateso ya kisaikolojia kuongezeka, wawili waliamua kuachana wasijue kuwa halikuwa jibu wala suluhu. Wakiwa kwenye mgogoro wao, aliingia mtu wa tatu ambaye hawakujua kuwa alikuwa sehemu ya mgogoro.

Punde, mtoto wao mkubwa aligundua tatizo lakini, naye kama wazazi wake, akaamua kukaa kimya asijaribu kuwakabili wazazi wake na kuuliza kunani. Hali hii ilimtafuna sana na kumsononesha sana hadi akajikuta amechanganyikiwa kutokana na alivyowapenda wazazi wake.

Kufupisha hadithi ndefu, mtoto huyu alijinyonga nje ya nyumba yao baada ya kushindwa kukubali kuwa wazazi wake walikuwa wameachana na kila mmoja kuchukua njia yake.

Tufanye nini?

Picha ya matukio hayo hapo juu inatuleta kwenye nini kifanyike. Kwanza, mkikosana msinuniane kwa muda mrefu. Kwani, si wa kwanza wala mwisho kukosana. Binadamu wote hukosana, hukabiliana, kukaa chini pamoja, au kuomba msaada na kutatua matatizo yao na maisha huendelea.

Pili, kama kununiana kunawapa fursa na namna ya kutatua tatizo, nunianeni kwa muda mfupi ili hasira zipoe halafu haraka sana muanze majadiliano ya kutatua tatizo.Wagombanao ndiyo wapatanao.

Tatu, kabla ya kuchukua hatua za kununiana, ni vizuri mkajua kuwa ukimya au kukwepa tatizo ni gonjwa baya sana na madhara yake ni makubwa mno.

Nne, mjue na kukikiri. Ndoa yenu si ya malaika wala mataahira wasiojitambua bali binadamu wenye akili na tabia tofauti.

 Hivyo, lazima mtakosana tu mtake msitake. Cha mno ni kukubali kuwa kukosana ni sehemu muhimu ya ubinadamu inayowawezesha kusababisha matatizo na kuyatatua kutokana na aina ya matatizo na welewa wa wahusika.

Tano, mjue kuwa kukosana ni fursa ya kubainisha tofauti na udhaifu wenu ambavyo huzaa ubora pale mnapoyakabili na kutayatua matatizo kwa njia zinazostahiki badala ya kukwepana au kununiana au kukaa kimya, kukomoana, au kususiana.

Katika maisha, migongano na tofauti ni mambo yasiyoepukika. Hata njiwa, pamoja na kusifika kwa upendo, hukosana na kuyamaliza.

Sita, mkikosana na kununiana msitegeane au kuviziana juu ya nani achukue hatua kwanza kuanza kutatua mgogoro kama wahusika hapo juu. Kwani, kunyamaziana au kuviziana ni ushahidi kuwa nyinyi ni wajinga ambao wanashindwa kujitambua, kutambuana, na kutambua matatizo yenu ili muyatatue.

Saba, ni vizuri kujichunguza na kuchunguzana na kupeana mirejesho ili kujua aina na ukubwa wa (ma)tatizo ili muweze kuyatatua pamoja kwa haki na na kuridhika. Hapa, lazima muwe wakweli katika kueleza mnavyoliona au kulijua tatizo ili iwe rahisi kupata ufumbuzi baada ya kujua ubora, udhaifu, kuelewa na hata kutoelewa tatizo.

Mwisho, msikimbiane mkidhani mnatatua tatizo wakati mnaliongeza ukubwa. Fanyeni kukosana kwenu kuwa fursa ya kujuana na kusaidiana katika maisha ya ndoa.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu08.107-08-2026
2Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026
3Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali01007-08-2026
4Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri01012-08-2026
5Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
6Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza01007-08-2026
7Не берите в жены разведенок с детьми! Из личного опыта! Читайте, чтобы ваша жизнь не превратилась в -5318-04-2026
8Tumtazame mwanamke kama injini ya maendeleo08.5709-08-2026
9TUONGEE KIUME: Ujumbe wenu huu hapa mnaojiita wanaume09.3209-08-2026
1010 анекдотов про брачный союз013.4727-07-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.