Soma hapa...
Mwanza. “Kwa siku sina mpangilio rasmi wa chakula, nakula kulingana na hali ya fedha ilivyo siku husika…”
Hivyo ndivyo anavyoanza kueleza Salvatory Masoja, akifafanua jinsi anavyopangilia chakula katika maisha yake ya kila siku hali ambayo kwa wengi inaweza kuonekana ya kawaida kabisa.
“Asubuhi nakunywa chai na chapati au supu na chapati, mchana wali na maharage na mboga za majani au ugali na dagaa… baadhi ya siku nakula mihogo. Usiku mara nyingi ni wali na maharage pia, nikibadilisha ni chapati tu na kinywaji chochote ila sio chai,” anasema.
Kwa upande mwingine, Justina Kulwa ana simulizi tofauti kidogo, lakini yenye taswira ileile ya mtindo wa maisha usiozingatia afya.
“Binafsi mimi si mpenzi sana wa kufanya mazoezi. Mara nyingi natumia bajaji kutoka Bulale hadi Buhongwa, kisha napanda daladala hadi mjini napofanyia kazi...mazoezi labda kusimama kwenye daladala napokosa kiti au kukimbilia gari. Vinginevyo mimi mazoezi ni mvivu sana,”anaeleza.
Simulizi hizi mbili zinaakisi maisha ya Watanzania wengi ambapo lishe bora si kipaumbele na mazoezi si sehemu ya ratiba ya kila siku. Wengi wanaishi kwa mazoea haya bila kufahamu kuwa wanajiweka katika hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukiza, hususan kisukari na shinikizo la damu yanayotajwa kuwatesa watu wengi duniania hasa barani Afrika.
Salvatory na Justina wanawakilisha kundi kubwa la watu katika jamii, ambao hawazingatii ulaji bora wala kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Sababu zinatofautiana; kwa baadhi ni hali ya kipato, kwa wengine ni ukosefu wa muda au maarifa, huku wengine ni mtazamo tu lakini bila kujali sababu, athari zake zinafanana.
Wataalamu wa afya wanasema kutokuwepo kwa mpangilio wa lishe, kunasababisha ulaji usio na uwiano wa virutubisho, huku kutofanya mazoezi kukichangia mwili kushindwa kutumia nishati ipasavyo. Hali hii huongeza uwezekano wa mtu kupata uzito kupita kiasi, na hatimaye magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani watu bilioni 1.4 duniani wanaishi na shinikizo la damu, sawa na karibu mtu mmoja kati ya watatu. Hata hivyo karibu asilimia 44 ya watu hawa hawajui kama wana ugonjwa huo.
Aidha, ni asilimia 23 tu ya wagonjwa wanaoweza kudhibiti shinikizo la damu ipasavyo.
Kwa upande wa kisukari, hali si tofauti. Ingawa makadirio ya awali yalionesha watu milioni 422 kuishi na ugonjwa huo, tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa idadi hiyo imeongezeka hadi zaidi ya watu milioni 800 duniani.
Ongezeko hili linahusishwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha hasa ulaji usiofaa na ukosefu wa mazoezi kwa ajili ya kuushughulisha mwili.
Mzigo unaoongezeka kwa kasi
Kwa hapa nchini, mzigo wa wagonjwa umeongezeka kutoka watu 6,502,913 mwaka 2024/2025 hadi kufikia 6,874,308 Machi 2026.
Gharama za matibabu nazo zimepanda kutoka Sh1.3 trilioni mwaka 2023 hadi Sh1.8 trilioni mwaka 2024 ikiashiria mzigo mkubwa kwa mfumo wa afya na uchumi kwa ujumla.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2026/2027, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa alieleza kuwa Serikali imeanzisha kliniki 130 za kisukari na shinikizo la damu na kufanya jumla kufikia 168 ili kunusuru maisha ya wananchi wanaotaabika na magonjwa hayo yanayotajwa pia sawa na muuaji wa kimyakimya.
Wataalamu wanasemaje?
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa lishe na mazoezi ni nguzo kuu katika kuzuia na kudhibiti magonjwa haya, huku moja ya malengo ya kimataifa kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, ikiwa ni kupunguza kiwango cha watu wenye shinikizo la damu lisilodhibitiwa kwa asilimia 25 kati ya mwaka 2010 na 2025.
Dk Michael Greger, daktari bingwa wa lishe kutoka Marekani na mwanzilishi wa taasisi ya NutritionFacts.org, anasema tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha wazi kuwa mabadiliko ya lishe, yanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa mujibu wa tafiti hizo ulaji wa sukari nyingi huongeza hatari ya kisukari, matumizi ya chumvi kupita kiasi huongeza shinikizo la damu na ukosefu wa mazoezi huathiri mfumo wa moyo na mishipa.
Kwa upande mwingine, ulaji wa mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara husaidia kudhibiti uzito na kuboresha afya kwa ujumla.
Changamoto ipo kwenye utekelezaji
Licha ya uelewa kuongezeka, bado watu wengi hawatekelezi, kwa Salvatory changamoto ni kipato na upatikanaji wa chakula bora, huku Justina ni mtazamo na ukosefu wa mazoea ya kufanya mazoezi.
Hii inaonyesha kuwa vita dhidi ya magonjwa haya haiwezi kuwa ya mtu mmoja mmoja pekee, bali inahitaji juhudi za pamoja kuanzia ngazi ya familia hadi sera za kitaifa.
Wataalamu wanashauri kuanza na hatua ndogo lakini za kudumu ikiwemo kupunguza ulaji wa sukari, chumvi na vyakula vya mafuta mengi, kuongeza ulaji wa mboga na matunda, kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku na kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.
Daktari wa tiba lishe katika Hospitali ya Kaloleni jijini Arusha, Dk Pendo Mushi anasema: “Usile chumvi nyingi, jaribu kutumia chini ya gramu mbili kwa siku. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi yaliyojaa, epuka kuvuta sigara au kutumia bidhaa za tumbaku, usinywe pombe kupita kiasi, ni vizui kikombe kimoja kwa siku kwa wanawake na viwili kwa wanaume lakini muhimu ni kwamba moja ya njia muhimu zaidi za kutibu kisukari, ni kudumisha mtindo wa maisha wenye afya,"
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 2 | Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu | 0 | 8.1 | 07-08-2026 |
| 3 | Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo | 0 | 10 | 10-08-2026 |
| 4 | Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri | 0 | 10 | 12-08-2026 |
| 5 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 6 | Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 7 | СМИ: у президентского дворца в столице Сомали слышна интенсивная стрельба | 0 | 0 | 25-04-2021 |
| 8 | Mwalimu auawa akizuia mifugo kupita eneo la shule | 0 | 6.05 | 29-07-2026 |
| 9 | В Забайкалье четыре человека заразились бруцеллезом | 0 | 0 | 30-09-2019 |
| 10 | Роспотребнадзор предупреждает: клещи продолжают атаковать смолян | 0 | 7 | 24-06-2026 |