Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Wadau wataka mipango ya tabianchi izingatie jinsia

Дата публикации: 20-02-2026 12:46:40

Wakati dunia ikiendelea kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, wadau wameonya kuwa vita hiyo haitakuwa na tija iwapo haitazingatia masuala ya kijinsia, hususan haki za afya ya uzazi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Februari 20, 2026

Wanafunzi wa shule ya msingi Nakasangwe  iliyopo Wazo Wilaya ya Kinondoni wakipanda miti ikiwa ni sehemu ya elimu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi chini ya mradi wa Kesho Njema.

By  Elizabeth Edward

Mwandishi

Mwananchi

Muktasari:
  • Tathmini ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi iliyofanyika kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2024/25 imeonyesha kujikita zaidi kwenye masuala ya miundombinu kama usafishaji wa mifereji na utunzaji wa mazingira, huku masuala ya haki za afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia yakikosa nafasi ya kutosha.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiendelea kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, wadau wameonya kuwa vita hiyo haitakuwa na tija iwapo haitazingatia masuala ya kijinsia, hususan haki za afya ya uzazi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Onyo hilo linakuja wakati tathmini ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika wilaya ya Kinondoni kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2024/25 ikionyesha kuwa juhudi nyingi zimejikita zaidi kwenye miundombinu kama usafishaji wa mifereji na utunzaji wa mazingira, huku mahitaji maalumu ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu yakiachwa pembezoni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika la My Legacy, Fortunata Temu, amesema makundi hayo yameendelea kubeba mzigo mkubwa wa athari za tabianchi, ikiwemo ukosefu wa maji safi, ongezeko la magonjwa na vitendo vya ukatili vinavyochochewa na mazingira magumu ya kiuchumi na kijamii.

Amesema kupitia mradi wa “Kesho Njema”, shirika hilo lilifanya tathmini katika kata za wilaya ya Kinondoni na kubaini kuwa mipango mingi ya tabianchi haijajumuisha mtazamo wa kijinsia ipasavyo.

“Wengi huwa wanaangalia athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye upande wa mazingira tu. Ukweli ni kwamba zipo athari nyingine ambazo zinawakumba moja kwa moja wanawake, watoto hata watu wenye ulemavu, lakini mipango iliyopo haingalii kwa jicho hilo.

“Tulibaini kuwa ushirikiano kati ya idara za mazingira, afya na jinsia bado ni mdogo. Pia, takwimu zilizogawanywa kijinsia hazitoshelezi, na ushiriki wa wanawake, vijana na makundi yaliyotengwa katika uamuzi wa tabianchi ni hafifu,” amesema Fortunata.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi ni ajenda mtambuka inayohitaji kuangaliwa kwa upana wake, akisisitiza umuhimu wa kuingiza viashiria vya haki za afya ya uzazi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia katika mikakati ya tabianchi kuanzia ngazi za mitaa.

Fortunata amesema ni muhimu pia kuimarisha uratibu wa kisekta na kutenga bajeti zinazozingatia jinsia ili kuhakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma katika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Programu wa shirika hilo, Amina Ally, amesema mbali na tathmini, mradi huo uliotekelezwa kwa mwaka mmoja kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, umewezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kukabiliana na athari za tabianchi kwa vitendo.

Mkurugenzi wa shirika la My Legacy Fortunata Temu (kushoto) akizungumza kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchini. Kulia ni mratibu wa programu Amina Ally.

Amesema miti 2,000 ya kivuli na matunda imepandwa katika shule 24 za Wilaya ya Kinondoni ili kupunguza joto na kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Wanafunzi pia wamepatiwa mafunzo ya upandaji na utunzaji wa miti, pamoja na matumizi ya mifumo rahisi ya umwagiliaji kwa kutumia chupa za plastiki zilizotumika, hatua inayosaidia kupunguza taka ngumu.

“Jumla ya wanafunzi 775 kutoka shule 25 wamefikiwa kupitia vilabu vya WASH kwa vipindi maalumu vya elimu ya tabianchi. Tumetumia mbinu shirikishi kama maigizo, hadithi na sanaa kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya nishati, uhifadhi wa mazingira na uhusiano wa tabianchi na masuala ya kijinsia,” amesema Amina.

Aidha, shirika hilo liliandaa mdahalo wa kijamii uliopewa jina la ‘Mgahawa wa Maarifa’ uliowakutanisha viongozi wa mitaa, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kujadili changamoto na suluhisho za tabianchi katika maeneo yao.

Akichangia katika mdahalo huo, mkazi wa Kawe, Richard Mtanga, amesema kuwa haitawezekana kuwa na mkakati madhubuti wa tabianchi bila kushughulikia kwa uzito masuala ya kijinsia.

“Hakuna mkakati madhubuti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi iwapo hautashughulikia ukatili wa kijinsia na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na haki zake. Ulinzi na utu lazima viwe sehemu ya hatua za kukabiliana na tabianchi,” amesema.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Kanisa Katoliki Zanzibar lawezesha wanawake mikopo isiyo na riba6819-07-2026
2Wakurugenzi wa Halmashauri wabebeshwa zigo la mazingira0717-01-2026
3Nishati mbadala yatajwa kuwa suluhu ya uharibifu wa mazingira2613-01-2026
4Serikali yaweka mfumo rahisi kwa wazalishaji5720-07-2026
5Министры труда G20 выступили за создание безопасных условий на рабочих местах для пожилых0002-09-2019
6SMZ yabadilisha mbinu ufuatiliaji huduma za afya kuimarisha uwajibikaji0520-07-2026
7ბინების შეძენა და რემონტი: ბათუმში ქალი თაღლითობაზე დააკავეს0517-07-2026
8Эксперты: женщины во всем мире сталкиваются с ограничением своих юридических прав0028-02-2019
9Лауреаты Нобелевской премии мира призвали страны изменить стратегию борьбы с наркотиками0022-09-2019
10ВОЗ призвала женщин детородного возраста отказаться от алкоголя0017-06-2021

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 5. Источник: www.mwananchi.co.tz.