Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Arteta apata wasiwasi majeraha ya Saka

Дата публикации: 22-10-2026 13:57:08

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, amepata hofu kwa majeraha ya mshambuliaji wake Bukayo Saka, akisema hali yake haionekani kuwa nzuri baada ya kulazimika kutoka uwanjani katika dakika ya 10, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 jana Jumatano, Oktoba 21, 2026.

Основное содержимое страницы с новостью.

Alhamisi, Oktoba 22, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Saka aliumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich wakati akijaribu kupiga pasi, hali iliyomlazimu Arteta kumtoa na kumuingiza Eberechi Eze, ambaye baadaye aliifungia Arsenal bao la kuongoza.

Munich, Ujerumani. Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, amepata hofu kwa majeraha ya mshambuliaji wake Bukayo Saka, akisema hali yake haionekani kuwa nzuri baada ya kulazimika kutoka uwanjani katika dakika ya 10, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 jana Jumatano, Oktoba 21, 2026.

Saka aliumia wakati akijaribu kupiga pasi, hali iliyomlazimu Arteta kumtoa na kumuingiza Eberechi Eze, ambaye baadaye aliifungia Arsenal bao la kuongoza.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Arteta alisema timu ya madaktari wa Arsenal imeonyesha wasiwasi kuhusu hali ya mshambuliaji huyo, ingawa uchunguzi zaidi unahitajika kubaini ukubwa wa jeraha lake.

“Wana wasiwasi kidogo. Mchezaji anapotoka uwanjani kutokana na maumivu makali ya ghafla, hiyo si habari njema. Hata hivyo, tunapaswa kusubiri na kuona,” amesema Arteta

Kocha huyo alitaja ratiba yenye msongamano wa mechi na kiwango kikubwa cha ushindani katika soka la kisasa kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuongeza changamoto kwa wachezaji.

Amesema mechi za kiwango cha juu zinahitaji nguvu nyingi, huku wachezaji wakilazimika kukimbia, kufuatilia wapinzani na kupambana katika kila eneo la uwanja kwa muda wote wa mchezo.

“Viwango vya nguvu vinavyohitajika katika mechi hizi ni vya ajabu. Huu ni mchezo ambao wachezaji wanakabiliana moja kwa moja kwa dakika 96. Kila tukio linahitaji nguvu na hakuna nafasi ya kupumua,” amesema.

Katika mchezo huo, Arsenal ilianza kwa kupata bao kupitia Eze, lakini Bayern ilisawazisha kupitia Alphonso Davies aliyefunga baada ya kupokea pasi kutoka kwa Harry Kane.

Kane baadaye aliifungia Bayern bao la pili kwa mkwaju wa penalti.

Arsenal ilionyesha moyo wa kupambana hadi dakika za mwisho, ambapo kiungo Declan Rice alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 82 na kuifanya timu hiyo iondoke na sare muhimu ugenini.

Hiyo ilikuwa mara ya pili tu kwa Arsenal katika historia ya Kombe la Ulaya na Ligi ya Mabingwa kufunga bao la kwanza, kisha kuruhusu wapinzani kuongoza kabla ya kuzuia kipigo. Mara ya kwanza ilikuwa Aprili 2024, pia dhidi ya Bayern Munich, katika mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Rice, aliyefunga bao lake la sita katika Ligi ya Mabingwa, amesema jambo hilo limempa furaha.

“Nina furaha sana. Gyokeres amekuwa na mchango mkubwa anapoingia akitokea benchi. Alifanya mikimbio mizuri na kunipa pasi ya kufunga bao,” amesema Rice.

Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Rice kufunga ugenini katika Ligi ya Mabingwa. Aidha, kiungo huyo alikuwa amehusika katika mabao matano katika mechi zake nane zilizotangulia kwenye mashindano yote, akifunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao.

Rice amesisitiza kuwa Arsenal haikwenda uwanjani kwa lengo la kujilinda pekee, licha ya kukabiliana na Bayern, ambayo aliitaja kuwa miongoni mwa timu bora barani Ulaya inapocheza nyumbani.

“Ni jambo ambalo kocha amekuwa akitufundisha. Hatutakuja hapa na kukaa nyuma tu. Bayern ni mojawapo ya timu bora barani Ulaya inapocheza nyumbani, hivyo kuja hapa na kuonyesha kiwango hiki ni jambo zuri sana. Tunapaswa kuendelea kupambana,” alisema.

Arsenal imeendelea pia kuonyesha uwezo wa kupata matokeo kupitia wachezaji wa akiba.

Timu hiyo imefunga mabao matano na pasi nne za mabao kutoka kwa wachezaji walioingia wakitokea benchi katika mashindano yote msimu huu.

Dhidi ya Bayern, Eze alifunga baada ya kuchukua nafasi ya Saka, huku Gyokeres akitoa mchango muhimu katika bao la kusawazisha la Rice.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Arsenal yaikomalia Bayern, Man United ikidhalilika012.4522-10-2026
2'It doesn't look good': Mikel Arteta sparks fears over Bukayo Saka injury after Arsenal winger limped off during 2-2 draw with Bayern Munich06.5221-10-2026
3Bukayo Saka is ruled out for up to EIGHT weeks in huge blow for Arsenal - but Mikel Arteta rejects fears that injury-hit star will suffer career burnout012.2223-10-2026
4PLAYER RATINGS: Bukayo Saka's performance hampered Arsenal in their Champions League defeat by Bayern Munich as another Gunners forward rates just 5.5/1009.6317-04-2024
5Arsenal slo tilbake mot Bayern – Ødegaard-assist i 2-2-kamp08.9521-10-2026
6Keinam pendele un fantastiska piespēle, "Arsenal" izvirzās vadībā un atspēlējas09.821-10-2026
7Bukayo Saka is OUT of Arsenal's squad to face Luton - as Mikel Arteta makes FIVE changes to his starting XI from their Manchester City stalemate06.9403-04-2024
8Сака возвращает лучшую форму в Арсенале! Друзья, вы это видели? ...07.8327-08-2026
9Mbappé amtetea Vinícius baada ya kuzomewa Real Madrid07.9822-10-2026
10"Бавария" примет "Арсенал" в Мюнхене 21 октября013.9820-10-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10.39. Источник: www.mwananchi.co.tz.