Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

DC Lugangira ataka uwajibikaji, uadilifu bima ya afya kwa wote

Дата публикации: 22-10-2026 18:47:08

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, amewataka viongozi na watumishi wa sekta ya afya kuzingatia uadilifu, uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila vikwazo.

Основное содержимое страницы с новостью.

Alhamisi, Oktoba 22, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, akizungumza leo Alhamisi, Oktoba 22, 2026, wakati akizindua awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla.

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • DC Neema amewataka viongozi na watumishi wa afya kuzingatia uadilifu, uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote. Katika awamu ya pili ya mpango huo mkoani Arusha, kaya 29,334 zenye wanufaika 80,909 zinatarajiwa kusajiliwa na kulipiwa michango ya bima na Serikali Kuu ili zipate matibabu bila vikwazo vya kifedha.

Arusha. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, amewataka viongozi na watumishi wa sekta ya afya kuzingatia uadilifu, uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila vikwazo.

Amesema viongozi wa wilaya, halmashauri na wataalamu wa afya katika ngazi zote wana wajibu wa kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kwa ufanisi na huduma zinawafikia wananchi wote kwa usawa na kwa wakati.

Lugangira ametoa kauli hiyo Alhamisi, Oktoba 22, 2026, wakati akizindua awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Kwa Mrombo, jijini Arusha.

Katika hotuba yake, Lugangira amesema viongozi wa ngazi zote wanapaswa kuhakikisha dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha huduma za afya inatekelezwa kwa vitendo, kwa kutoa huduma bora zinazomfikia mwananchi wa kawaida.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, akizungumza leo Alhamisi, Oktoba 22, 2026, wakati akizindua awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla.

Kuwalinda wananchi

Lugangira amesema Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote hauna ubaguzi, hivyo unapaswa kuwafikia wananchi wa makundi mbalimbali, wakiwemo wakulima, wafugaji, wafanyabiashara wadogo, waendesha bodaboda, vijana, wazee na wanawake wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Amesema mpango huo unalenga kulinda ustawi wa familia kwa kupunguza mzigo wa gharama za matibabu, ambao umekuwa ukichangia umasikini unaotokana na maradhi.

Ameeleza kuwa Serikali inalenga kuondoa hali inayowalazimu wananchi kuuza mali na rasilimali zao za familia au kukopa fedha na kuingia kwenye madeni makubwa ili kugharamia matibabu wanapougua.

Katika kutimiza azma hiyo, Lugangira amewataka viongozi na watendaji wa sekta ya afya kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinakuwa tayari wakati wote kuhudumia wananchi wanaofika kupata matibabu.

Kaya 29,334 kulipiwa bima

Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Arusha, Hipoliti Lello, amesema Serikali imeweka kipaumbele kwa kaya maskini na zisizo na uwezo wa kiuchumi ili ziweze kunufaika na mpango huo.

Lello amesema katika Mkoa wa Arusha, jumla ya kaya 29,334 zenye wanufaika 80,909 zimepangwa kusajiliwa katika awamu hiyo.

Ameeleza kuwa Serikali Kuu itagharamia michango yote ya bima kwa kaya hizo zilizoorodheshwa, hatua inayolenga kuziwezesha kupata matibabu bila kikwazo cha kifedha.

Utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote unatarajiwa kuongeza idadi ya wananchi wanaonufaika na huduma za bima ya afya mkoani Arusha, huku ukilenga kupunguza athari za gharama za matibabu kwa kaya zenye uhitaji.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Bima ya Afya kwa Wote II kulenga kaya 625,00005.9822-10-2026
2Namtumbo watakiwa kuachana na kuni, mkaa05.5318-09-2026
3Uelewa chumvi yenye madini joto tatizo kwa wengi05.5622-10-2026
4Власти Приамурья готовы увеличить "подъемные" сельским фельдшерам и докторам0017-02-2020
5Володин: средства госбюджета должны обеспечивать граждан качественной медпомощью0005-11-2021
6Губернатор НАО взял под контроль оптимизацию кадров в здравоохранении региона0017-12-2021
7Мурашко отметил, что беременные нуждаются в особом внимании в период пандемии0028-06-2021
8Модернизацию первичного звена здравоохранения в Иркутской области оценили в 98 млрд рублей0019-02-2020
9Расходы на медицину в 2020 году в Архангельской области выросли на 36%0024-03-2021
10Архангельские депутаты обсудили масштабный капремонт социальной сферы05.8917-09-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 4.73. Источник: www.mwananchi.co.tz.