Upatikanaji wa chumvi yenye madini joto katika kaya na kwa wauzaji wa chakula cha mtaani umeimarika katika Wilaya ya Nyamagana, Mwanza, lakini uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa madini hayo bado ni mdogo, hali inayoweza kudhoofisha juhudi za kupambana na matatizo ya kiafya yanayotokana na upungufu wake.
Ijumaa, Oktoba 23, 2026

Uongezaji wa chumvi kwenye chakula umetajwa kuchangia matumizi makubwa ya bidhaa hiyo. Picha na mtandao
Dar es Salaam. Upatikanaji wa chumvi yenye madini joto katika kaya na kwa wauzaji wa chakula cha mtaani umeimarika katika Wilaya ya Nyamagana, Mwanza, lakini uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa madini hayo bado ni mdogo, hali inayoweza kudhoofisha juhudi za kupambana na matatizo ya kiafya yanayotokana na upungufu wake.
Utafiti uliofanyika wilayani humo umebaini kuwa kati ya sampuli 417 za chumvi zilizopimwa, sampuli 399 sawa na asilimia 95.7 zilikuwa na madini hayo, huku sampuli 355, sawa na asilimia 85, zikiwa na kiwango cha kutosha cha madini.
Hata hivyo, licha ya upatikanaji huo, ni asilimia 51.1 pekee ya washiriki walioweza kutaja kwa usahihi angalau kazi moja ya madini hayo mwilini, huku asilimia 32.6 tu wakitambua angalau chanzo kimoja cha chakula chenye madini hayo.
Utafiti huo uitwao: ‘Assessment of Knowledge and Availability of Iodine in Table Salt among Households and Street Vendors in Nyamagana District, Mwanza, Tanzania’ na kuchapishwa kwenye jarida la Tanzania Medicaka mwaka huu, ulilenga kutathmini uelewa wa wananchi kuhusu madini joto na upatikanaji wa chumvi yenye madini hayo.
Utafiti ulitumia mbinu mchanganyiko za ukusanyaji wa taarifa, ukiwahusisha washiriki 417 katika sehemu ya takwimu na wengine 30 katika sehemu ya mahojiano ya kina.
Matokeo yalionyesha kuwa chumvi iliyofungashwa ilikuwa na kiwango kikubwa zaidi cha upatikanaji wa madini joto, huku sampuli zote 342 zilizopimwa, sawa na asilimia 100, zikiwa na madini hayo.
Kwa upande wa chumvi isiyofungashwa, sampuli 45 kati ya 46, sawa na asilimia 97.8, zilikuwa na madini joto. Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti kwa chumvi ghafi, ambapo sampuli 16 kati ya 29, sawa na asilimia 55.2, zilikuwa na madini hayo.
Uelewa mdogo tatizo
Licha ya upatikanaji mkubwa wa chumvi yenye madini joto, utafiti umebaini kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu kazi za madini hayo mwilini.
Kati ya washiriki 417, watu 265, sawa na asilimia 63.5, walikuwa wamewahi kusikia kuhusu madini hayo. Hata hivyo, ni washiriki 217, sawa na asilimia 51.1, walioweza kutaja kwa usahihi angalau kazi moja ya madini hayo.
Uelewa kuhusu vyakula vinavyopatikana kwa wingi wa iodini ulikuwa mdogo zaidi, ambapo ni asilimia 32.6 pekee ya washiriki walioweza kutaja angalau chanzo kimoja cha chakula chenye madini hayo.
Utafiti pia umebaini kuwa uelewa kuhusu makundi ya watu yanayohitaji madini hayo kwa kiwango kikubwa zaidi ulikuwa mdogo, ambapo ni asilimia 8.9 tu ya washiriki waliweza kuyatambua.
Hali hiyo inaonyesha kuwa upatikanaji wa chumvi yenye madini hayo pekee, hautoshi kuhakikisha wananchi wanaelewa umuhimu wa madini hayo na namna ya kuyatumia kwa usahihi.
Dhana potofu
Matokeo ya mahojiano ya kina pia yalibaini kuwepo kwa dhana potofu kuhusu chumvi yenye madini joto, ikiwamo imani kuwa ina kemikali zinazoweza kudhuru afya na kwamba chumvi ghafi ni bora zaidi kuliko ile iliyoongezewa madini.
Dhana hizo zinaweza kuwafanya baadhi ya wananchi kuepuka kutumia chumvi hiyo, licha ya umuhimu wake katika afya ya mwili.
Upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa la afya ya umma duniani, na ni miongoni mwa sababu zinazoweza kuzuilika za kudhoofika kwa uwezo wa utambuzi na maendeleo ya ubongo.
Madini hayo yana umuhimu katika utengenezaji wa homoni za tezi ya thyroid, ambazo husaidia kudhibiti ukuaji na maendeleo ya mwili.
Upungufu wa iodini unaweza kusababisha kuvimba kwa tezi ya thyroid, hali inayojulikana kama goita, na kuathiri maendeleo ya ubongo, hasa kwa watoto wanaokua.
Tanzania ilianza kutekeleza mpango wa kuhakikisha chumvi yote inayotumiwa na wananchi inaongezewa madini joto mwaka 1994, kwa lengo la kupunguza matatizo ya kiafya yanayotokana na upungufu wa madini hayo.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Namtumbo watakiwa kuachana na kuni, mkaa | 0 | 5.53 | 18-09-2026 |
| 2 | Safari ya nishati safi inavyokumbana na mikingamo | 0 | 5.95 | 24-08-2026 |
| 3 | Shule ya Kalangalala kutumia nishati safi | 0 | 6.87 | 27-08-2026 |
| 4 | DRC; madini, fedha na gharama ya vita-3 | 0 | 10 | 22-10-2026 |
| 5 | DC Lugangira ataka uwajibikaji, uadilifu bima ya afya kwa wote | 0 | 4.73 | 22-10-2026 |
| 6 | Министр ископаемых Танзании призвал прекратить политизацию алмазной промышленности | 0 | 0 | 27-07-2023 |
| 7 | Liberia: Govt Discussing to Revamp Western Cluster Mining Project | 0 | 9.66 | 13-10-2026 |
| 8 | Naberera walalamikia tembo kuua mtoto na kuharibu mazao | 0 | 6.4 | 22-10-2026 |
| 9 | Wahandisi wajifungia kusuka mikakati utatuzi changamoto za viwanda, ajira | 0 | 5.95 | 22-10-2026 |
| 10 | В Черногорске планируют в 2020 году начать ликвидацию горной выработки шахты №8 | 0 | 0 | 25-09-2019 |