Licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, kuwataka madereva kurejea kazini na kuendelea na safari kwa amani, baadhi ya abiria wameendelea kusota katika Kituo cha Mabasi Magufuli wakisubiri hatima ya safari zao.
Jumanne, Septemba 29, 2026

Dar es Salaam. Licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, kuwataka madereva kurejea kazini na kuendelea na safari kwa amani, baadhi ya abiria wameendelea kusota katika Kituo cha Mabasi Magufuli wakisubiri hatima ya safari zao.
Baadhi ya abiria waliokuwa wamekatia tiketi jana Jumatatu Septemba 28, 2026 na leo Jumanne, wamesema wameahidiwa kuanza safari kesho Jumatano, muda ambao walipaswa kuwa wameondoka leo, huku wengine wakisema hawajapewa taarifa kuhusu lini wataondoka na hivyo kuendelea kuwa katika sintofahamu.

Hali hiyo imeendelea kutawala kituoni hapo saa chache baada ya Waziri Katambi kuzungumza na madereva waliogoma kutoa huduma tangu asubuhi, wakishinikiza Serikali kutatua changamoto wanazodai kukabiliana nazo.
Waziri Katambi aliwataka madereva kuanza safari kwa amani, huku akiwahakikishia ulinzi katika maeneo yote watakayopita na kufanya shughuli zao.

Hata hivyo, kauli hiyo haijabadilisha mara moja hali ndani ya kituo hicho, ambacho hadi usiku huu kimeendelea kuonekana kama yadi ya kuegesha mabasi.
Abiria wameonekana wamekaa katika makundi, huku wengine wakilala kwenye viti na chini wakisubiri hatima ya safari zao. Baadhi wameendelea kukaa ndani ya mabasi tangu asubuhi, wakitumia simu, kulala au kuzungumza na wenzao.
Sabina Musemwa, mmoja wa abiria waliokwama kituoni hapo, amesema alifika saa 12 asubuhi na alitarajiwa kuondoka saa tano asubuhi, lakini safari yake ilishindikana kutokana na mgomo huo.
Amesema baadaye waliambiwa wasubiri hadi kesho, siku ambayo walipaswa kuwa tayari wameanza safari.

“Nasubiri, nalala kwa kujikunja hapa hapa nikisubiri kesho kama tulivyoahidiwa kwenda Shinyanga na basi la Katarama. Niko na wenzangu, ingawa kuna wengine wameenda kulala lodge,” amesema.
Sabina amesema hali hiyo imekuwa ikiwapa wakati mgumu, lakini hawana namna nyingine kwa kuwa tayari wameshakata tiketi na hawana uhakika kama fedha zao zinaweza kurejeshwa.
Abdazari John amesema bado wapo kwenye sintofahamu licha ya kupewa ahadi ya kuondoka kesho, akisema dalili za safari kuanza bado hazionekani.

“Kila dereva unayemuona ni kama hajafurahishwa na uamuzi uliotolewa. Tulikuwa na matumaini baada ya Waziri kuzungumza na madereva kwamba labda wangeridhia na sasa hivi tungekuwa barabarani, lakini kama unavyoona, nipo na familia yangu hapa,” amesema.
Hadi habari hii inaandikwa saa 5 usiku wa leo Jumanne, hakuna basi lililokuwa limetoka kituoni hapo wala kuonyesha dalili ya kuanza safari.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Katambi asitisha kukata pointi, awataka madereva kurejea kazini | 0 | 5.7 | 29-09-2026 |
| 2 | Rais Samia ateua Ma DC 22 wengine 26 wahamishwa, Ma DED na DAS hawa hapa | 0 | 15.69 | 29-09-2026 |
| 3 | Malipo ya meza Mbagala bado kizungumkuti | 0 | 10 | 28-09-2026 |
| 4 | Mgomo wa madereva watesa Mwanza, binti akosa usaili wa kazi Dar | 0 | 4.96 | 29-09-2026 |
| 5 | Wadau watafuta suluhu changamoto zinazotishia afya ya vijana | 0 | 5.26 | 29-09-2026 |
| 6 | Kenya: Mizani Poll - Ruto Leads Kalonzo, Sifuna in Presidential Preference Survey | 0 | 11.24 | 25-09-2026 |
| 7 | Nigeria: Congo Adopts NCDMB's Policies to Develop Oil and Gas Sector | 0 | 7.55 | 28-09-2026 |
| 8 | Mayele aweka mikakati mipya TRA United | 0 | 8.56 | 26-09-2026 |
| 9 | Fikiri: Simba, Yanga zimetujenga | 0 | 6.55 | 26-09-2026 |
| 10 | Fullt krig i Tigray efter ny offensiv mot Abiy Ahmed | 0 | 7.13 | 25-09-2026 |