Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Mayele aweka mikakati mipya TRA United

Дата публикации: 26-09-2026 14:06:20

MSHAMBULIAJI wa TRA United, Kassim Shaibu ‘Mayele’ amesema licha ya ugeni wake katika kikosi hicho ila hadi sasa kuna maendeleo mazuri, ingawa amekiri anapaswa kupambana ili kuendana na ushindani mkubwa kutoka kwa washambuliaji wenzake.

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Daudi Elibahati

Reporter

Mwananchi Communications Limited

MSHAMBULIAJI wa TRA United, Kassim Shaibu ‘Mayele’ amesema licha ya ugeni wake katika kikosi hicho ila hadi sasa kuna maendeleo mazuri, ingawa amekiri anapaswa kupambana ili kuendana na ushindani mkubwa kutoka kwa washambuliaji wenzake.

Nyota huyo alijiunga na TRA United, Julai 25, 2026 kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kuachana na Mtibwa Sugar ambayo imeshuka daraja kufuatia kikosi hicho kumaliza nafasi ya 15 na pointi 27, katika Ligi Kuu kwa msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayele alisema licha ya kupewa dakika chache za kucheza ila anaendelea kuzoea mazingira na jinsi ya kutengeneza muunganiko mzuri na washambuliaji wenzake, jambo linalompa nguvu ya kupambana ili acheze pia zaidi.

“Kwa dakika chache ninazoendelea kuzipata nataka nihakikishe nazitumia vizuri, kwa sasa tuna benchi pia jipya la ufundi, hivyo ni wakati wa kila mchezaji kuonyesha kipaji chake ili ashawishi kupewa nafasi zaidi uwanjani,” alisema Mayele.

Aidha, mshambuliaji huyo alisema licha ya kutofunga bao lolote hadi sasa la Ligi Kuu Bara, ila bado hajakata tamaa kwa sababu ni mapema, huku lengo lake kubwa ni kuhakikisha anafanya vizuri zaidi na kuivunja rekodi ya msimu wa 2025-2026.

Kwa msimu wa 2025-2026, katika Ligi Kuu Bara akiwa na Mtibwa Sugar, Mayele alihusika na mabao matatu kati ya 25 yaliyofungwa na kikosi hicho, baada ya mshambuliaji huyo kufunga mawili na kuchangia bao lingine moja kwa maana ya kutoa asisti.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Baleba njia yake Man United yahitaji subira08.0625-09-2026
2Fikiri: Simba, Yanga zimetujenga06.5526-09-2026
3Neema Kusekwa: Mgore, Manula wampa maujanja07.6626-09-2026
4Rais wa CAF afunguka ishu ya Afcon 2027 kuondolewa Tanzania02019-09-2026
5Lamine: Mbappe na mimi ndo bora zaidi duniani08.4425-09-2026
6Singeli 'kichaka' kinachompa maisha D Voice06.4826-09-2026
7MO Salah aivuruga Misri07.9226-09-2026
8Basata yamshushia rungu Dudu Baya, mratibu wa Bongo Flava 30010.3426-09-2026
9Rany Kida; King of Dance mwenye simulizi moto ya dansi09.0724-09-2026
10Mhilu mambo safi Geita Gold011.526-09-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.56. Источник: www.mwanaspoti.co.tz.