NYOTA wa Misri na Trabzonspor, Mohamed Salah ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa huku kukiwa na taarifa za mvutano katika kikosi hicho baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Angola katika mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Mwananchi Communications Limited
Cairo, Misri: NYOTA wa Misri na Trabzonspor, Mohamed Salah ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa huku kukiwa na taarifa za mvutano katika kikosi hicho baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Angola katika mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Salah, ambaye ni nahodha wa timu hiyo, alitolewa dakika ya 60 na Kocha Hossam Hassan, uamuzi ambao umeibua maswali miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka Misri.
Baada ya mechi hiyo, Hassan alisisitiza kumtoa Salah hakukutokana na majeraha, bali ulikuwa uamuzi wa kiufundi. Kocha huyo hakutoa dalili nyota huyo alikuwa na tatizo lolote la kiafya.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Misri, Ahmed Abdel Basset, Salah ameondoka kambini kwa utulivu huku akikwepa kuhusishwa na mgogoro wowote unaodaiwa kuibuka katika kikosi.
Taarifa hizo zinaeleza kumekuwa na hali ya sintofahamu ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, huku baadhi ya kauli zilizotolewa baada ya mchezo dhidi ya Angola zikichochea zaidi mjadala kuhusu kinachoendelea katika kikosi hicho.
Sare hiyo imeongeza presha kwa Misri, ambayo ilitarajiwa kuanza kampeni yake ya kufuzu AFCON 2027 kwa ushindi ikiwa nyumbani au ugenini dhidi ya Angola. Badala yake, ilishindwa kupata bao katika dakika zote 90.
Hassan sasa anakabiliwa na jukumu la kurekebisha mambo ndani ya timu kabla ya mchezo wake unaofuata dhidi ya Sudan Kusini, unaotarajiwa kuchezwa Septemba 29.
Mchezo huo utakuwa muhimu kwa Misri katika harakati zake za kuwania tiketi ya AFCON 2027, lakini pia utakuwa kipimo kwa Hassan kuhusu namna atakavyodhibiti hali ndani ya kikosi chake.
Wakati huo huo, macho yataelekezwa kwa Salah na kama atarejea kambini au kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za kuondoka kwake. Hadi sasa, hakuna maelezo rasmi kutoka Shirikisho la Soka Misri kuhusu hatua hiyo.
Kwa sasa, taarifa za mvutano ndani ya kambi zimeongeza presha kwa Hassan, huku Misri ikihitaji ushindi dhidi ya Sudan Kusini ili kurejesha hali nzuri katika kampeni yake ya kufuzu AFCON.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Rais wa CAF afunguka ishu ya Afcon 2027 kuondolewa Tanzania | 0 | 20 | 19-09-2026 |
| 2 | Ufunguzi Kombe la Dunia 2026 Mexico | 0 | 8.07 | 12-06-2026 |
| 3 | Ahmedy Ally aipiga mkwara Yanga mastaa wa Simba wakienda Sauz kwa makundi,jeuri ya MO Dewji | 0 | 10 | 25-09-2026 |
| 4 | Mbappé aumia goti, kuikosa mechi ya Ubelgiji | 0 | 5.89 | 26-09-2026 |
| 5 | Baleba njia yake Man United yahitaji subira | 0 | 8.06 | 25-09-2026 |
| 6 | Nicolas Batum asema inatosha! | 0 | 7.89 | 26-09-2026 |
| 7 | Paredi la Arsenal latikisa mitaa ya London | 0 | 12.45 | 01-06-2026 |
| 8 | USA-Perù, Musah titolare con la maglia numero 10 | 0 | 20.51 | 26-09-2026 |
| 9 | Kanuni mpya EPL zaanza kupunguza upotezaji muda uwanjani | 0 | 9.9 | 26-09-2026 |
| 10 | Verso Crotone-Salernitana: il prepartita di Serse Cosmi | 0 | 16.9 | 25-09-2026 |