Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Majeshi Afrika Mashariki kutoa huduma hizi Tanzania

Дата публикации: 26-08-2026 13:13:35

Majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yameanza kutoa huduma mbalimbali za kijamii na kibinadamu kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo matibabu ya bure kutoka kwa madaktari bingwa wa nchi za Burundi, Somalia, Tanzania, Rwanda, Kenya, na Uganda.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumatano, Agosti 26, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lawa mwenyeji wa Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Ushirikiano wa Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yaliyoanza leo Agosti 26, hadi Septemba Mosi, 2026 hapa nchini.

Dar es Salaam. Majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yameanza kutoa huduma mbalimbali za kijamii na kibinadamu kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo matibabu ya bure kutoka kwa madaktari bingwa wa nchi za Burundi, Somalia, Tanzania, Rwanda, Kenya, na Uganda.

Hatua hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Ushirikiano wa Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo yaliyoanza leo Agosti 26, hadi Septemba Mosi, 2026 hapa nchini.

Aidha, maadhimisho hayo yanahusisha shughuli za ukarabati na utoaji wa misaada ya kijamii katika vituo vya afya, vituo vya kulelea watoto yatima, na Magereza katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Arusha, na Zanzibar.

Baadhi ya vituo vitakavyonufaika na huduma na ukarabati huo ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Hospitali ya Vijibweni Kigamboni, na Kituo cha Afya Yombo Malawi (Dar es Salaam), Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi na Hospitali ya Wilaya Bagamoyo (Pwani), pamoja na Hospitali za Wilaya za Mwerapongwe Unguja na Vitongoji Pemba.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Jumatano, Agosti 26, 2026, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Salum Haji Othman amesema ushiriki wa majeshi kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ni ishara ya umoja wa kikanda na dhamira ya majeshi hayo ya kuhudumia wananchi.

"Tanzania inafurahia kuwa mwenyeji wa vikosi kutoka Burundi, Kenya, Uganda, Somalia na nchi nyingine washirika ushirikiano huu unaimarisha uhusiano kati ya majeshi na wananchi pamoja na kubadilishana uzoefu katika operesheni mbalimbali," ameeleza.

Mnadhimu huyo Mkuu wa JWTZ amesema ushirikiano unawawezesha wanajeshi kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu, kuimarisha utayari na kuongeza uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja.

“Licha ya mipaka yetu ya kitaifa, sisi ni eneo moja lililoungana katika kuwatumikia wananchi,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Utawala wa JWTZ, Brigedia Jenerali Dk Agatha Katua amebainisha kwamba zoezi hilo siyo la kwanza kwani kwa upande wa Tanzania ni mara ya pili kwa kuwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka 2022.

"Kwa mwaka huu Septemba Mosi ndio siku tunayo timiza miaka 62 ya jeshi la JWTZ. Kwa hiyo wiki moja kabla tunafanya moja ya njia za kuadhimisha ni pamoja na kuwa na zoezi hili ambalo linashirikisha majeshi ya nchi za Afrika Mashariki kutoa huduma kwa jamii ili kujenga mahusiano mazuri na jamii zinazotuzunguka" ameelezea.

Kupitia zoezi hilo, misaada itawafikia wafungwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam na Gereza la Kisongo Mkoani Arusha, sambamba na vituo vya kulelea watoto yatima vya Kurasini, Mwandaiwa Orphanage Centre Bunju, Chanika Children Shelter (Dar es Salaam), SOS Orphanage Centre Zanzibar, na vituo vya afya vya Kibokoni Pemba na Mapinduzi Dodoma, Chamwino.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1China kuisaidia Tanzania usimamizi mashirika ya umma04.5626-08-2026
2Tanzania Chairs Regional Labour Migration Committee06.0818-08-2026
3MBEGU YA UCHUMI: Kugeuza umeme wa ziada kuwa fursa ya kiuchumi      07.327-08-2026
4Koffi Olomide ana historia ndefu Tanzania08.2628-08-2026
5РФ обсуждает с некоторыми странами заключение договоров о выдаче преступников0006-05-2025
6Несырьевой неэнергетический экспорт Москвы в Африку за восемь месяцев вырос в 1,5 раза0017-11-2021
7Magoti azindua kampeni chanjo ya polio Kisarawe07.327-08-2026
8UCHAMBUZI WA MJEMA: Tusijidanganye, tunahitaji maandalizi haya kabla ya 2030018.3327-08-2026
9Культурно-деловые миссии Петербурга пройдут в 2024 году в четырех странах Африки0031-07-2023
10Страны БРИКС надеются на устойчивое урегулирование конфликта на Украине0029-04-2025

Классификация: Пресс-релизы. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 4.64. Источник: www.mwananchi.co.tz.