Mwanamuziki nguli kutoka DRC, Koffi Olomide, ni moja ya wasanii ambao wanahistoria ndefu na Tanzania. Huku akiwa amekanyaga ardhi ya Tanzania zaidi ya mara 20 kwa ajili ya shughuli za kimuziki.
Dar es Salaam. Mwanamuziki nguli kutoka DRC, Koffi Olomide, ni moja ya wasanii ambao wanahistoria ndefu na Tanzania. Huku akiwa amekanyaga ardhi ya Tanzania zaidi ya mara 20 kwa ajili ya shughuli za kimuziki.
Koffi alitua Bongo kwa mara ya kwanza mwaka 1993 na kukutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Club Billicanas and Casino Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulikuwa sehemu ya shughuli za kumtambulisha rasmi kwa mashabiki wa Tanzania na kuitangaza albamu yake ya Noblesse Oblige. Iliyokuwa na nyimbo zilizofanya vizuri, ikiwemo Papa Plus.
Koffi hakuwa peke yake, bali alitua na wanamuziki wa bendi yake ya Quartier Latin, akiwemo mpiga gitaa mahiri Beniko Popolipo.Mkutano huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo promota Tamukati Ndongala, Ronnie Mtawali na wengineo.
Tangu ziara hiyo ya kwanza, Koffi ameendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania. Miongoni mwa ziara zake ni ya Machi 2020, alipokuja Dar es Salaam kwa ajili ya tamasha la Mahaba ya Rhumba lililofanyika Mlimani City.

Wakati huo, Koffi alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena baada ya kuwasili nchini na kueleza furaha yake ya kurejea Tanzania.
Ziara hiyo pia ilifungua ukurasa mwingine muhimu katika uhusiano wake na wasanii wa Tanzania. Koffi alieleza kumkubali Nandy na kuupenda wimbo wake Kivuruge, jambo lililopelekea wawili hao kufanya kolabo katika wimbo wa Leo Leo, uliotoka Februari 11, 2021.
Katika safari hiyo ya kimuziki, Koffi alionekana jukwaani pamoja na Nandy na Cindy kwenye tamasha lake la Mahaba ya Rhumba. Huku wakitumbuiza pamoja wimbo wa Kivuruge Remix.

Lakini kabla ya hapo, jina la Koffi lilikuwa tayari limeanza kutambulika na mashabiki wa Bongo ambapo mwaka 2020 alitua nchini kwa ajili ya kufanya kazi na Diamond Platnumz kupitia wimbo wa ‘Waah!’ ulioachiwa Novemba 2020.
Waah ambapo video yake imeshatazamwa mara milioni 201 katika mtandao wa YouTube ilikuwa kolabo kubwa iliyounganisha Bongo Fleva na muziki wa Kongo. Wimbo huo uliimbwa kwa Kiswahili na Lingala na ulitengenezwa Tanzania baada ya Koffi kukaa nchini kwa takribani wiki moja.
Wimbo huo ulikimbiza Youtube ukifikisha zaidi ya watazamaji milioni moja ndani ya saa nane na milioni mbili ndani ya saa 24. Jambo lililoifanya kuwa miongoni mwa nyimbo kutoka Afrika zilizovunja rekodi kwa wakati huo.

Ushirikiano wa Diamond na Koffi haukuishia hapo. Miaka mitatu baadaye, walirejea tena studio na kuachia wimbo wa Achii, uliotoka Agosti 15, 2023.
Hivyo basi licha ya kutua Bongo mara nyingi zaidi, mpaka kufikia sasa amefanikiwa kufanya kolabo tatu tu na mastaa wa Tanzania ambao ni Nandy ‘Leo Leo’, Waah! na Achii, akishirikiana na Diamond Platnumz.
Zaidi ya nyimbo hizo, ziara zake zimekuwa sehemu ya historia ya namna muziki wa Kongo ulivyokutana na Bongo Fleva katika vipindi tofauti. Koffi akiwa mmoja wa mastaa wakubwa wa rumba na soukous, ujio wake Tanzania umeendelea kuimarisha uhusiano wa kimuziki kati ya Dar es Salaam na Kinshasa.
Koffi amekuwa akikubalika Zaidi kupitia ngoma zake mbalimbali ikiwemo Loi, Fouta Djallon, Héros National, Effrakata, Ekoti té (Selfie) na nyinginezo.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Safari ya K Zungu hadi kutumbuiza Yanga | 0 | 6.85 | 28-08-2026 |
| 2 | Salif Keita agoma kufanya tamasha Afrika Kusini | 0 | 7.72 | 28-08-2026 |
| 3 | Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 4 | Mapato Stendi ya Magufuli yapaa | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 5 | Makamua afichua kinachoendelea ndani ya Wakali Kwanza | 0 | 6.27 | 26-08-2026 |
| 6 | MBEGU YA UCHUMI: Kugeuza umeme wa ziada kuwa fursa ya kiuchumi | 0 | 7.3 | 27-08-2026 |
| 7 | Waliopata ajira mtandaoni kupatiwa mikopo | 0 | 9.33 | 27-08-2026 |
| 8 | Kinachofuata kwa Dk Nchimbi | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 9 | Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 10 | Dolly Parton alikuwa na mawigi 350 | 0 | 10.42 | 28-08-2026 |