Shirikisho la Mpira wa Miguu Ufaransa (FFP) limempa Zinedine Zidane mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Ufaransa (FFP) limempa Zinedine Zidane mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Zidane anachukua mikoba iliyoachwa na Didier Deschamps ambaye kibarua chake cha kuinoa Ufaransa kilifikia tamati baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo timu hiyo iliishia katika nafasi ya nne.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari za Michezo, Fabrizio Romano, FFP itamtambulisha Zidane hivi karibuni.
"Zidane atakuwa kocha wa Ufaransa hadi Juni 2030. Habari imethibitishwa na Zizou atatangazwa kuwa Kocha Mkuu siku zijazo. Anarudi kazini akiwa na Ufaransa," ameandika Romano.
Kiungo huyo wa zamani wa Juventus na Real Madrid, ana vibarua vitatu mbele yake ambavyo ni mashindano ya Ligi ya Ulaya mwakani, Kombe Kombe la Ulaya 2028 na Kombe la Dunia 2030.
Zidane, mwenye umri wa miaka 54, hajashika nafasi yoyote ya ukocha tangu alipoondoka Real Madrid mwaka 2021, baada ya kuhudumu kwa mara ya pili kama kocha wa klabu hiyo kubwa ya Hispania.
Katika kipindi chake akiwa Real Madrid, alitwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya mwaka 2016 na 2018.
Pia alishinda mataji mawili ya La Liga pamoja na makombe mengine kadhaa ya ndani na ya kimataifa.
Zidane sasa anakuwa mchezaji wa pili aliyekuwepo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kilichotwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 1998 kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo kama ilivyo kwa mtangulizi wake Didier Descham
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Зидан подписал долгосрочный контракт со сборной Франции | 5 | 5 | 21-07-2026 |
| 2 | Зинедин Зидан возглавил сборную Франции | 5 | 7 | 21-07-2026 |
| 3 | Зидан станет новым главным тренером сборной Франции | 5 | 7 | 14-07-2026 |
| 4 | Зидан станет новым главным тренером сборной Франции | 0 | 5 | 15-07-2026 |
| 5 | Появились подробности о назначении Зидана в сборную Франции | 5 | 7 | 17-07-2026 |
| 6 | Легендарный футболист и тренер возглавит сборную Франции | 5 | 7 | 17-07-2026 |
| 7 | Зидан отказал нескольким клубам и выбрал новую команду | 5 | 7 | 15-07-2026 |
| 8 | СМИ: Зинедин Зидан может возглавить сборную Франции | 0 | 0 | 13-02-2021 |
| 9 | Didier Deschamps quitte les Bleus : pourquoi la succession s'annonce comme un "cadeau empoisonné" pour Zinedine Zidane ? | -3 | 6 | 10-07-2026 |
| 10 | Enosh kutoka ukedi kwenye gofu hadi Tanzania One | 0 | 7 | 20-07-2026 |