Soma zaidi hapa...
Alhamisi, Oktoba 22, 2026

Dar es Salaam. Miili ya Humphrey Msoka (66) na mpwa wake, Dickson Msoka (24), imezikwa huku viongozi wa dini wakikemea mauaji na vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Humphrey aliuawa Oktoba 18, 2026, nyumbani kwake Kibamba, jijini Dar es Salaam, akidaiwa kushambuliwa kwa mapanga na Dickson, ambaye alikuwa akiishi naye.
Wawili hao wameagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kibwegere Adonai, kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kanisa Katoliki Kibwegere.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaaga marehemu hao leo Alhamisi, Oktoba 22, 2026, mchungaji wa kanisa hilo, Peter Zebedayo, amekemea kitendo cha Dickson kumuua baba yake mkubwa, akikitaja kuwa ni jambo ovu lisilopaswa kuvumiliwa katika jamii.

Wakati majeneza yenye miili ya Hunfrey Msoka anaedaiwa kuuawa kwa kupigwa mapanga na mtoto wa ndugu yake aitwaye Dickson Msoka ambaye nae aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira yakitoka Kanisani Kibwegere eneo la Kibamba Shule Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kanisa la RC. Picha na Said Powa
“Tunakemea vikali kitendo kilichofanywa na ndugu yetu Dickson kumshambulia baba yake mkubwa. Sisi viongozi wa kiroho tunakikemea vikali sana, ni jambo ovu sana,” amesema.
Hata hivyo, mchungaji huyo amekemea pia vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi, akisema hatua iliyochukuliwa na baadhi yao baada ya tukio hilo ilisababisha kifo cha Dickson.
Amesema ingawa baadhi ya wananchi walikuwa na nia ya kutafuta haki ya Humphrey, njia waliyoitumia haikupaswa kusababisha kupotea kwa maisha ya mtu mwingine.
“Pia, tunakemea na kuiomba jamii ifuate sheria, miongozo na utu. Kitendo kilichofanywa na wananchi wenye hasira kali na kusababisha kifo cha Dickson, kwa upande mmoja, kilionekana kuwa ni kutafuta haki ya Humphrey.
“Njia iliyotumika imesababisha kupoteza maisha ya Dickson. Tunakemea vitendo hivyo ili jamii iendelee kuwa na amani,” amesema.
Zebedayo amewakumbusha wananchi umuhimu wa kuhudhuria ibada.
Amewataka viongozi wa vyama vya siasa kutumia majukwaa yao kuhamasisha wananchi kuhudhuria ibada.
Miili haikufunguliwa
Katika hali isiyo ya kawaida, miili ya marehemu hao haikufunguliwa ili waombolezaji waweze kuwaaga. Badala yake, picha zao ziliwekwa juu ya majeneza, huku waombolezaji wakiruhusiwa kuaga kwa kutazama picha hizo pekee.

Majeneza yenye miili ya Hunfrey Msoka anaedaiwa kuuawa kwa kupigwa mapanga na mtoto wa ndugu yake aitwaye Dickson Msoka ambaye nae aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira yakiwa kwenye makaburi ya RC Kibwegere eneo la Kibamba Shule Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuzikwa. Picha na Said Powa
Pia, wakati wa kusoma wasifu wa marehemu hao, utaratibu wa ndugu au mwakilishi wa familia kusoma wasifu haukutumika. Mshehereshaji, Chimwemwe Chiwaya, ndiye aliyesaidia familia katika jukumu hilo.
Akisoma wasifu wa Humphrey, Chiwaya amesema marehemu alikuwa na watoto wawili na wajukuu watano.
Alizaliwa mkoani Kilimanjaro na hadi mauti yanamkuta alikuwa akiishi Mtaa wa Hondogo Kimbaga, Dar es Salaam.
Amesema Humphrey alikuwa mjasiriamali na ameacha mjane.
Kwa upande wa Dickson, Chiwaya amesema alikuwa mjasiriamali aliyezaliwa Mtaa wa Hondogo, jijini Dar es Salaam, na hakuwa na mke wala watoto.
Amesema kabla ya kifo chake, Dickson aliugua na baadaye akapata hali ya kuchanganyikiwa, ambayo ilitangulia tukio hilo.
Akitoa salamu za rambirambi, Ernest Mgawe, mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Hondogo na mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Ubungo, amesema tukio hilo limewaumiza wakazi wengi.
“Tunatoa pole kwa wana-Hondogo wote kwa msiba huu ambao kila mmoja ameumizwa nao. Msiba unapotokea, kila mmoja anakuwa na majonzi makubwa sana. Wana-Hondogo, msiba huu utukumbushe kuwa maisha ya duniani ni ya kupita, na mambo ya kuzingatia ni kuishi kwa kumcha Mungu na kupendana,” amesema.
Mgawe amewataka wananchi kuepuka kufungiana barabara, akisema tabia hiyo imeibuka miongoni mwao, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha upendo.
Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Hondogo amesema chama hicho kimepata pigo kwa kumpoteza kada wake mwaminifu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Hondogo, Leonard Sabuni amesema bado wanajiuliza sababu iliyomfanya Dickson kutenda tukio hilo, akieleza kuwa hakujua kuwepo kwa changamoto kati ya wawili hao.
“Nimeishi nao kwa zaidi ya miaka 20, sijawahi kuona shida yoyote. Hawa ni majirani zangu wa muda mrefu. Watoto wake wanakuja kwangu na wangu wanakwenda kwake. Hata wake zetu wanatembeleana. Tutamkumbuka Humphrey,” amesema.
Kumbukumbu ya tukio
Mtoto wa pili wa Humphrey, Herman Msoka, aliiambia Mwananchi Oktoba 19, 2026 kuwa tukio la kuuawa kwa baba yake lilitokea Oktoba 18, 2026, saa mbili usiku.
Herman amesema kabla ya tukio hilo, baba yake alimkumbusha Dickson umuhimu wa kunywa maji mengi kutokana na maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) aliyokuwa nayo.
Kwa mujibu wa Herman, baada ya mazungumzo hayo, Dickson alimwita Humphrey ndani ya nyumba, kisha akamshambulia kwa panga kichwani na mkononi.
Herman amesema muda mfupi kabla ya tukio hilo, Dickson alikuwa akizungumza na baba yake mkubwa na kumwomba amsaidie kutupa simu yake chooni, kisha amchome kisu ili aende Kituo cha Polisi Segerea.

Wakati majeneza yenye miili ya Hunfrey Msoka anaedaiwa kuuawa kwa kupigwa mapanga na mtoto wa ndugu yake aitwaye Dickson Msoka ambaye nae aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira yakitoka Kanisani Kibwegere eneo la Kibamba Shule Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kanisa la RC. Picha na Said Powa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi kuhusu chanzo chake unaendelea.
Kwa mujibu wa Muliro, Humphrey alifariki kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa, huku Dickson akifariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kushambuliwa na wananchi waliokasirishwa na tukio hilo.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu | 0 | 8.1 | 07-08-2026 |
| 2 | Yanayowasubiri wahitimu mitaani | 0 | 0 | 20-07-2026 |
| 3 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 4 | Mapya yaibuka mahakamani, wakili wa Lissu atokwa machozi | 0 | 5 | 20-07-2026 |
| 5 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 6 | Rais Mwinyi atangaza ufadhili wanafunzi watakaopata daraja la kwanza Zanzibar | 0 | 10 | 21-10-2026 |
| 7 | Ilborians wanavyoikumbuka Ilboru Personality na maisha ya kande | 0 | 10 | 21-09-2026 |
| 8 | DRC; madini, fedha na gharama ya vita-3 | 0 | 10 | 22-10-2026 |
| 9 | Baba Rossie Uisso: afunguka mazito juu ya ushindi wa mwanae | 0 | 10 | 16-10-2026 |
| 10 | ICC yashinda Tuzo ya Sakharov | 0 | 10 | 22-10-2026 |