Mtuhumiwa wa mauaji ya wanawake wawili waliokutwa wamefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni jijini Mbeya, Benson Steven, maarufu Mkembo, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Alhamisi, Oktoba 22, 2026

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga akizungumza leo Oktoba 22, 2026 kuhusu tukio la mauaji
By Sadam Sadick
Mwananchi Communications Limited
Mbeya. Mtuhumiwa wa mauaji ya wanawake wawili waliokutwa wamefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni jijini Mbeya, Benson Steven, maarufu Mkembo, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Mtuhumiwa huyo alijeruhiwa kwa risasi baada ya kujaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, alipokuwa akiongoza askari kuelekea nyumbani kwa mganga wa jadi anayedaiwa kumpa masharti ya kufanya mauaji hayo kwa imani za kishirikina.
Akizungumza leo Alhamisi, Oktoba 22, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amesema tukio la kukutwa kwa miili hiyo liliripotiwa Oktoba 16, saa 11:45 alfajiri, katika Mtaa wa Makunguru jijini humo.
Amesema mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni, Nice Kabuje, ndiye aliyetoa taarifa polisi baada ya kukuta miili ya wanawake wawili.
Kwa mujibu wa Kuzaga, askari walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi, ambapo mwili mmoja ulitambuliwa kuwa wa Annastazia Mwakipesile, mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kabwe, huku mwingine ukiwa haujatambuliwa na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Amesema miili hiyo ilikutwa ikiwa imefichwa chini ya kitanda katika chumba kilichoitwa Ufilipino ndani ya nyumba hiyo ya kulala wageni.
“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina kwa lengo la kupata utajiri, kwani mtuhumiwa alieleza kabla ya kufanya mauaji hayo alienda kwa mganga,” amesema Kuzaga.
Ameongeza kuwa mtuhumiwa alikubali kuwaongoza askari hadi nyumbani kwa mganga huyo wa jadi. Hata hivyo, wakiwa njiani, mtuhumiwa aliruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia.
Kuzaga amesema askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha, lakini aliendelea kukimbia, ndipo askari mmoja alipofyatua risasi iliyompata kwenye paja la mguu wa kushoto.
Amesema mtuhumiwa alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, lakini alifariki dunia akiwa bado anaendelea kutibiwa.
Kuzaga ameeleza kuwa Mkembo aliwahi kukamatwa Temeke, Dar es Salaam, na kushtakiwa kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba. Alitiwa hatiani na kufungwa jela mwaka mmoja, kisha kurejea Mbeya baada ya kumaliza kifungo chake.
Pia, amesema Desemba 29, 2025, mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Iwambi, Mbeya, akiwa na watu wengine wanane na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha. Hata hivyo, waliachiliwa huru baada ya mlalamikaji kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi kutokana na kuugua.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Naberera walalamikia tembo kuua mtoto na kuharibu mazao | 0 | 6.4 | 22-10-2026 |
| 2 | Mapato Stendi ya Magufuli yapaa | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 3 | Bunge kumthibitisha Ndejembi leo | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 4 | Two Dead, 21 Hurt in Head-On Crash On Limbe-Zomba Road | 0 | 16.4 | 22-07-2026 |
| 5 | Kenya confirms its first Ebola case and death in a man who traveled from Congo | 0 | 6.61 | 07-10-2026 |
| 6 | Huduma za dharura zapunguza vifo hospitalini kwa asilimia 31 Tanzania | 5 | 7 | 02-07-2026 |
| 7 | Два человека скончались после группового отравления алкоголем в Туве | 0 | 9.22 | 30-08-2026 |
| 8 | В Туве два человека погибли от отравления спиртом | 0 | 8.62 | 30-08-2026 |
| 9 | Пенсионерка погибла при столкновении двух авто в российском регионе | 0 | 7.23 | 16-10-2026 |
| 10 | Namtumbo watakiwa kuachana na kuni, mkaa | 0 | 5.53 | 18-09-2026 |