Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Gachagua akataa shinikizo la kujiunga na Muungano wa Ukombozi

Дата публикации: 29-09-2026 16:31:23

Chama cha Democracy for Citizens Party (DCP) kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, kimepinga wito wa kujiunga na muungano wa Ukombozi, kikisema kinataka kwanza kujenga nguvu yake ya kisiasa kabla ya kufanya mazungumzo na vyama vingine vya upinzani.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumanne, Septemba 29, 2026

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Msimamo huo umekiweka DCP katika mvutano na kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, ambaye ni mratibu wa muungano huo.

Nairobi. Chama cha Democracy for Citizens Party (DCP) kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, kimepinga wito wa kujiunga na muungano wa Ukombozi, kikisema kinataka kwanza kujenga nguvu yake ya kisiasa kabla ya kufanya mazungumzo na vyama vingine vya upinzani.

Msimamo huo umekiweka DCP katika mvutano na kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka, ambaye ni mratibu wa muungano huo.

Muungano wa Ukombozi ulizinduliwa Septemba 21, 2026, ukiwa ni zao la muungano wa Azimio wa mwaka 2022 ambao Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliujenga katika jitihada ambazo hazikufanikiwa za kumsukuma marehemu Raila Odinga kushinda urais.

Musyoka amesema muungano huo unalenga kuvishirikisha vyama zaidi, kikiwemo DCP.

Hata hivyo, DCP inaonekana kutokuwa tayari kujiunga na muungano huo wakati ushindani ukiongezeka kuhusu nani anayeongoza kisiasa eneo la Mlima Kenya na nani anayepaswa kuwa na sauti kubwa katika kuamua mkakati wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027.

Mshirika wa karibu wa Gachagua ameliambia gazeti la Nation kwamba Kenyatta hapaswi tena kutafuta nafasi ya msingi katika shughuli za kisiasa za upinzani.

“Kenyatta anapaswa kujiondoa katika mjadala wa kisiasa. Kitu pekee kutoka kwake tunachoweza kukubali ni fedha zake. Anaweza kubaki na kitu kingine chochote anachoamini anaweza kutoa,” amesema kiongozi huyo.

Kenyatta alisema Septemba 22 kwamba pendekezo la kumpa nafasi kiongozi wa Jubilee, Fred Matiang’i, katika Muungano wa Ukombozi lilikuwa bado ni pendekezo tu na kwamba yeye ataiwakilisha Jubilee katika meza ya mazungumzo ya muungano huo.

Badala ya kujiunga mara moja na Ukombozi, DCP inajipanga kama nguvu huru ya kisiasa ambayo itafanya mazungumzo na vyama vingine ikiwa katika nafasi yenye nguvu.

Kauli za hadharani za chama hicho zinaonyesha kwamba kinataka kutofautisha kati ya vyama ambavyo vinaona kuwa vina wafuasi wengi katika uchaguzi na vile ambavyo vinaviona kuwa havina uzito mkubwa kisiasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Watu Mashuhuri la DCP, Maina Kamanda amesema chama hicho kinaamini kinaweza kukusanya zaidi ya kura milioni nane, hivyo kujiunga na muungano kutahitaji kuchunguza kwa makini kile ambacho vyama vingine vinaweza kuleta mezani.

“Gachagua amewakusanya wapigakura wengi wa Mlima Kenya chini ya DCP. Amefikia pia jamii za Maa na Kipsigis. Yeye ni harakati ya kitaifa peke yake. Kutuambia tujiunge na muungano kutahitaji kwanza tufanye uchunguzi,” amesema.

Kamanda amesema kwa sasa DCP inawachukulia Gachagua, Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, waziri wa zamani, Eugene Wamalwa na Musyoka kuwa ni viongozi wa upinzani wenye ushawishi mkubwa kisiasa.

“DCP inawatambua Gachagua, Edwin Sifuna, Eugene Wamalwa na Kalonzo Musyoka pekee kuwa viongozi wakuu wenye ushawishi. Hatutajifanya kwa muda mrefu wala kujificha kutokana na ukweli huo milele,” alisema.

Msimamo huo pia umeungwa mkono katika wiki za hivi karibuni na Gavana wa Murang’a, Irungu Kang’ata; Mbunge wa Kajiado North, Onesmus Ngogoyo; Mbunge wa Naivasha, Jane Kihara; na Mbunge wa Manyatta, Gitonga Mukunji.

Aliyekuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Kitaifa la Jubilee, Pauline Njoroge, pia amesisitiza kuwa upinzani unahitaji kundi dogo la viongozi wakuu wenye ushawishi wa kisiasa unaoweza kuthibitishwa.

“Upinzani huu hauhitaji meza isiyoisha ya viongozi wakuu… unahitaji kituo kidogo na kinachoaminika. Vyama vyote vinavyounda muungano viketi katika Baraza la Vyama vya Muungano kama ilivyo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa—kila mmoja anashiriki, lakini wachache wanaoketi katika Baraza la Usalama hutoa uhalali,” amesema.

Njoroge amesema uanachama katika kundi la viongozi wakuu haupaswi kutegemea tu kuwa mtu anamiliki chama cha siasa, bali unapaswa kuzingatia ushawishi wa kitaifa unaoweza kuthibitishwa na uungwaji mkono katika maeneo mbalimbali.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Kenya: Kenyan News Site Citizen Digital Didn't Publish Article Claiming Dcp Leader Gachagua's Endorsements Triggered Defections02.9829-09-2026
2Kenya: Disregard Fake Newspaper Front Page Claiming There Are Calls for Kenyan President Ruto and His Ex-Deputy Gachagua to Reconcile05.529-09-2026
3Rais Samia ateua Ma DC 22 wengine 26 wahamishwa, Ma DED na DAS hawa hapa015.6929-09-2026
4Kenya: Mizani Poll - Ruto Leads Kalonzo, Sifuna in Presidential Preference Survey011.2425-09-2026
5Singeli 'kichaka' kinachompa maisha D Voice06.4826-09-2026
6Fikiri: Simba, Yanga zimetujenga06.5526-09-2026
7Anahtar Parti Genel Başkanı Yavuz Ağıralioğlu: 'Cumhurbaşkanlığı için herkesten iddialıyım'06.2728-09-2026
8Africa: Ruto Unveils $600m Clean Cooking Investment Opportunity, Nairobi to Host 2027 Africa Summit09.923-09-2026
9Liberia: 'Opposition Is Not CDC Property'06.1729-09-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 6.08. Источник: www.mwananchi.co.tz.