Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Ronaldo akosa bao, atolewa

Дата публикации: 25-09-2026 09:08:49

CRISTIANO Ronaldo amekumbana na usiku wa kukatisha tamaa katika kurejea kwake Lisbon, baada ya kukosa nafasi kadhaa na baadaye bao lake kukataliwa na VAR kwa sababu ya kuotea, huku Ureno ikiichapa Wales 1-0 katika Ligi ya Mataifa.

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Septemba 25, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Communications Limited

Muktasari:
  • Ronaldo, 41, aliondoka uwanjani akiwa bado na mabao 979 katika maisha yake ya soka, yakiwamo 146 aliyofunga akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

LISBON, Ureno. CRISTIANO Ronaldo amekumbana na usiku wa kukatisha tamaa katika kurejea kwake Lisbon, baada ya kukosa nafasi kadhaa na baadaye bao lake kukataliwa na VAR kwa sababu ya kuotea, huku Ureno ikiichapa Wales 1-0 katika Ligi ya Mataifa.

Ronaldo, 41, aliondoka uwanjani akiwa bado na mabao 979 katika maisha yake ya soka, yakiwamo 146 aliyofunga akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Joao Felix katikati ya kipindi cha kwanza, baada ya shuti lake la umbali wa takribani mita 18 kugonga mchezaji wa Wales na kubadili mwelekeo kabla ya kuingia wavuni.

Mchezo huo ulikuwa na mvuto wa kipekee kwa Ronaldo, ambaye alianza safari yake ya soka la kulipwa kwenye Uwanja wa Jose Alvalade miaka 24 iliyopita akiwa na Sporting Lisbon, kabla ya baadaye kujiunga na Manchester United.

Kabla ya mchezo, mjadala mkubwa ulihusu mustakabali wake katika soka la kimataifa, huku Ronaldo akijiwekea lengo la kufikisha mabao 1,000 kabla ya kustaafu.

Lakini hakufanikiwa kuongeza bao lolote katika usiku huo. Katika kipindi cha kwanza, alikosa nafasi nne, kabla ya kupoteza nafasi nyingine nzuri kipindi cha pili pale mpira ulipomgonga mguuni akiwa umbali wa takribani mita tano kutoka langoni.

Muda mfupi baadaye, Ronaldo alidhani amefunga bao lake la 980, lakini furaha yake ilikatizwa baada ya VAR kubaini alikuwa ameotea na kulifuta bao hilo.

Ronaldo, aliyekuwa akicheza mchezo wake wa 234 katika timu ya taifa, alishangiliwa kwa nguvu kila alipogusa mpira na mashabiki waliokuwa wamefurika Uwanja wa Jose Alvalade.

Alianza kuwatia hofu Wales dakika ya 10 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Felix, lakini shuti lake la mguu wa kushoto kutoka upande wa pembeni lilitoka nje.

Dakika chache baadaye alipata nafasi nyingine nzuri, lakini Neco Williams aliokoa kwa kuzuia shuti hilo na kuutoa mpira kuwa kona.

Ureno, iliyokuwa na wachezaji watano waliowahi kushinda Ligi ya Mabingwa na watatu waliowahi kuteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or akiwamo Bruno Fernandes, Nuno Mendes na Vitinha iliendelea kutawala mchezo katika mwanzo wa enzi ya kocha Jorge Jesus.

Beki wa Manchester City, Ruben Dias, alikosa nafasi ya kichwa baada ya mpira wake kupita juu ya lango, kabla ya winga wa Chelsea, Pedro Neto, kupiga shuti lililotoka nje akiwa kwenye nguzo ya mbali.

Wales, licha ya kushinikizwa, iliweza kuhimili dakika 20 za mwanzo, huku mshambuliaji wa Liverpool, Lewis Koumas, akionyesha uwezo mzuri wa kuushikilia mpira mbele.

Hata hivyo, Felix alivunja ukuta huo katikati ya kipindi cha kwanza baada ya Nuno Mendes kumpita Ethan Ampadu na kumpa pasi akiwa umbali wa takribani mita 27 kutoka langoni.

Felix, aliyewahi kucheza Chelsea, alipiga shuti la mguu wa kulia kutoka nje ya eneo la hatari, lakini mpira uligonga beki Ben Davies na kubadili mwelekeo kabla ya kumpita kipa Danny Ward na kutinga wavuni.

Hata hivyo, Ward alionekana kuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika kuzuia shuti hilo.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Mbappé aumia goti, kuikosa mechi ya Ubelgiji05.8926-09-2026
2Baleba njia yake Man United yahitaji subira08.0625-09-2026
3Paredi la ubingwa UEFA CL, PSG yateka jiji la Paris08.0201-06-2026
4Lamine: Mbappe na mimi ndo bora zaidi duniani08.4425-09-2026
5UEFA yaonya soka Ulaya, yagawanyika08.4425-09-2026
6Мбаппе выбыл из-за травмы колена011.8926-09-2026
7Мбаппе выбыл из-за травмы колена на неопределенный срок012.3426-09-2026
8Болельщик выбежал на поле по окончании прощального матча Вагнера Лава05.6326-09-2026
9Роналдиньо обратился к Вагнеру Лаву перед прощальным матчем за ЦСКА07.2226-09-2026
10Nicolas Batum asema inatosha!07.8926-09-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 6.88. Источник: www.mwanaspoti.co.tz.