Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Ngorongoro yapoteza kwa penalti fainali CECAFA-20

Дата публикации: 24-09-2026 15:26:52

Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, imepoteza fainali ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa penalti 4-3, baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan, mchezo uliopigwa jana Alhamisi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Основное содержимое страницы с новостью.

Alhamisi, Septemba 24, 2026

Mchezaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes wakati akijaribu kumzuia mchezaji wa Sudan katika mechi ya fainali ya CECAFA. Picha na Mtandao

By  Nevumba Abubakar

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, imepoteza fainali ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa penalti 4-3, baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan, mchezo uliopigwa leo Alhamisi, Septemba 24, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ngorongoro, iliyokuwa bingwa mtetezi baada ya kutwaa ubingwa mwaka 2024, ilianza kufungwa dakika ya 93, kabla ya Abdulnasir Abdallah ‘Casemiro’ kusawazisha dakika ya 115 kwa kumalizia pasi ya Farid Mzalendo. Wachezaji hao wote waliingia kipindi cha pili wakitokea benchi.

Tanzania na Sudan, ambazo tayari zilikuwa zimefuzu Fainali za AFCON U-20 zitakazofanyika Ghana mwaka 2027 baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali, ziliingia Uwanja wa Uhuru zikiwa na lengo la kumaliza kampeni kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA.

Tanzania iliingia fainali ikiwa imeshinda mechi zake zote tatu bila kuruhusu bao, huku Sudan ikiwa imefunga mabao sita katika michezo yake ya mashindano hayo.

Katika mchezo huo, kila upande ulionekana kuwa makini zaidi kutofanya makosa ambayo yangeipa timu pinzani nafasi ya kushambulia. Kocha wa Ngorongoro, Mario Rivera Campesino, na mwenzake wa Sudan, Salaheldin Ahmed, waliweka mkazo katika kulinda maeneo muhimu na kuzuia mipango ya wapinzani wao kabla ya kuongeza nguvu katika mashambulizi.

Ngorongoro, iliyokuwa imefunga mabao tisa katika mechi tatu zilizopita, haikupata nafasi nyingi za kufunga kama ilivyokuwa katika michezo dhidi ya Rwanda, Ethiopia na Burundi.

Kwa Sudan, ambayo ilionyesha uwezo wa kubadilisha mchezo katika ushindi wake wa mabao 3-2 dhidi ya Uganda, ilikutana na Ngorongoro iliyokuwa makini katika kuzuia mashambulizi.

Hali hiyo ilifanya eneo la kiungo kuwa sehemu muhimu ya mchezo, huku timu zote zikijaribu kutawala mchezo bila kuacha mianya ambayo ingeweza kutumiwa na wapinzani kupata bao. Kila upande ulipofanikiwa kuvuka mstari wa kiungo wa mpinzani, safu ya ulinzi ilifanya kazi ya kuzima mashambulizi kabla hayajawa hatari, jambo lililofanya mchezo mwingi uchezwe kwa tahadhari huku kila timu ikisubiri kosa la mpinzani.

Kadiri dakika zilivyokuwa zikisonga, badala ya kuona timu zikifunguka na kushambulia kwa nguvu, mchezo uliendelea kuwa wa kusubiri. Makocha waliendelea kufanya marekebisho ya kiufundi huku kila mmoja akijaribu kumsoma mwenzake na kucheza kwa tahadhari hadi mwamuzi alipomaliza dakika 90 kwa matokeo ya 0-0.

Suluhu hiyo iliifanya fainali kuwa tofauti na mechi mbili za nusu fainali zilizokuwa na mabao mengi, ambapo Tanzania iliifunga Burundi 2-0 na Sudan ikaichapa Uganda 3-2.

Tanzania na Sudan tayari zilikuwa zimehakikisha nafasi za kushiriki AFCON U-20 mwaka 2027 nchini Ghana, hivyo fainali hiyo ilikuwa ni nafasi ya kusaka ubingwa wa CECAFA baada ya tiketi ya AFCON kuwa tayari mikononi mwao.

Katika mchezo mwingine wa kuwania nafasi ya tatu, Uganda iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burundi na kutwaa medali ya shaba katika michuano hiyo.

Uganda ilianza kwa kasi na kuonekana kuwa na kiu zaidi ya ushindi, ambapo Derrick Ssozi aliipa timu hiyo bao la kwanza dakika ya 22 baada ya kumalizia pasi ya chini iliyotolewa na Elvis Opakrwoth ndani ya eneo la hatari.

Burundi ilijaribu kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Uganda pamoja na kipa Adrian Isabirye waliendelea kuzuia mashambulizi hayo. Uganda nayo ilipata nafasi kadhaa za kuongeza bao kabla ya mapumziko, lakini haikuzitumia.

Kyakuwa alifunga bao la pili dakika za mwisho baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Steven Oyirwoth, hivyo kuifungia Uganda ushindi wa mabao 2-0 na kuhakikisha inamaliza mashindano ikiwa nafasi ya tatu.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Burundi Book Semi-Final Place As Sudan Make Strong Start in TotalEnergies CAF U-20 Afcon Cecafa Qualifier08.0118-09-2026
2Wachezaji Harambee Stars wagomea mazoezi kisa posho05.9224-09-2026
3Kenya: Kenya's Junior Starlets Earn Another Historic FIFA U17 World Cup Qualification5713-07-2026
4Namibia: Young Warriors Make History With Winning Streak06.8724-09-2026
5Rais Mwinyi afichua kilichofanikisha maridhiano Zanzibar01025-09-2026
6Сборная Сенегала по футболу второй раз подряд вышла в финал Кубка африканских наций0002-02-2022
7East Africa: Malawi Host South Sudan in AFCON Qualifier As Pressure Mounts On Coach Pasuwa09.1924-09-2026
8Египетские футболисты обыграли команду Зимбабве в стартовом матче Кубка африканских наций0022-06-2019
9Сборная Камеруна по футболу стала первым полуфиналистом Кубка африканских наций0029-01-2022
10Сборная ДР Конго обыграла Узбекистан и вышла в плей-офф ЧМ5528-06-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.64. Источник: www.mwananchi.co.tz.