Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Fedha za Watanzania nje zafikisha Sh4 trilioni

Дата публикации: 26-08-2026 14:36:33

Fedha zilizotumwa nchini na Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia benki na simu zimeongezeka hadi Sh4.44 trilioni mwaka 2025 kutoka Sh2.95 trilioni mwaka 2024.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumatano, Agosti 26, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Ripoti hiyo iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa kati ya fedha zilizotumwa nchini, Sh2.29 trilioni mwaka 2025 zilipitia benki ikiwa ni ongezeko kutoka Sh1.89 trilioni mwaka 2024, huku miamala iliyopitia kwenye simu ikiongezeka hadi Sh1.75 trilioni kutoka Sh1.07 trilioni mwaka uliotangulia.

Dar es Salaam. Fedha zilizotumwa nchini na Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia benki na simu zimeongezeka hadi Sh4.44 trilioni mwaka 2025 kutoka Sh2.95 trilioni mwaka 2024.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya National Payment Systems Annual Report 2025 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ripoti hiyo inaeleza Sh2.29 trilioni zilitumwa kupitia benki mwaka 2025, kutoka Sh1.89 trilioni mwaka 2024. Fedha zilizotumwa kupitia simu ziliongezeka hadi Sh1.75 trilioni kutoka Sh1.07 trilioni.

BoT imesema ongezeko hilo limechangiwa na maboresho ya mfumo wa malipo wa haraka (Tanzania Instant Payment System-TIPS), unaowezesha fedha kutoka nje kuingia moja kwa moja katika akaunti za benki na pochi za simu za wapokeaji nchini.

Mfumo huo pia umelenga kupunguza ucheleweshaji na gharama za uhamishaji fedha za kimataifa, huku ukiongeza uwazi katika miamala ya kuvuka mipaka.

Ongezeko hilo limeenda sambamba na ukuaji wa matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu. Watumiaji waliongezeka kutoka milioni 63.2 mwaka 2024 hadi milioni 75.8 mwaka 2025, huku mawakala wakiongezeka kutoka milioni 1.48 hadi milioni 1.98.

Mkurugenzi wa Diaspora Tanzania, Kelvin Nyamori, amesema ongezeko la fedha hizo limechangiwa zaidi na juhudi za Watanzania wenyewe kuliko mikakati maalumu ya Serikali ya kuwawezesha kupata ajira katika masoko ya nje.

Amesema Tanzania haijaweka juhudi za kutosha kuwatafutia wananchi ajira nje ya nchi, tofauti na baadhi ya mataifa, likiwamo Kenya.

“Kwa Tanzania ni ngumu kuongezeka kwa sababu hakuna jitihada zozote ambazo zinawasaidia wananchi kwenda kufanya kazi huko. Hata hiki kidogo kinachokuja wanapaswa kupongezwa kwani ni juhudi zao wenyewe,” amesema.

Nyamori amesema Tanzania pia haijatumia kikamilifu fursa ya fedha hizo kuelekeza katika uwekezaji na shughuli za uzalishaji.

“Nchi nyingine zina taratibu za kurejesha fedha hizi kwa njia ya kodi, si tu zile zinazokuja kusaidia ndugu. Sisi tumechelewa sana. Tufungue fursa tuone namna gani watu wanaofanya kazi huko wanaweza kurudisha fedha huku,” amesema.

Amesema uraia pacha unaweza kurahisisha Watanzania wanaoishi nje kuwekeza nchini, badala ya kukabili changamoto za hadhi ya uraia, viza na vibali wanapokuja Tanzania.

Kwa upande wake, Festus Mussa, anayeishi Marekani, amesema Serikali inapaswa kuongeza jitihada za kuwawezesha Watanzania kupata ajira nje na kuwatambua ili wanufaike na fursa zinazopatikana.

“Tukifanya hivi tutakuwa tumeweka mazingira mazuri kwa wananchi wanaofanya kazi nje ya nchi, wanayoweza kupata fedha nzuri na hata kinachorudi nyumbani kikaongezeka zaidi,” amesema.

Serikali imeanza kuweka mifumo ya kuwaunganisha Watanzania na ajira za nje, ambapo 1,432 walipata ajira kati ya Novemba 2025 na Januari 2026.

Lengo ni kufikisha fursa hizo hadi ajira 8,000 za kimataifa na kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, ukiwemo kupata takwimu za idadi yao, nchi wanazokwenda na aina ya kazi wanazofanya.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Waliopata ajira mtandaoni kupatiwa mikopo09.3327-08-2026
2Mobile Money Reshapes Economy016.6217-08-2026
3China kuisaidia Tanzania usimamizi mashirika ya umma04.5626-08-2026
4Минфин предлагает расширить расходы на нацпроекты и реализацию посланий президента0020-06-2022
5Tanzania's Digital Rise - What the Latest Tcra Report Tells Us07.4417-08-2026
6Доходы бюджета Чувашии на 2025 год увеличили на 2,3 млрд рублей0002-10-2025
7В Татарстане сообщили о росте объема инвестиций минимум на 10% в 2025 году0019-12-2025
8Бюджет Забайкалья на 2025 год увеличили на 7,3 млрд рублей0020-11-2025
9Расходы бюджета на льготные ипотечные программы составят почти 279 млрд рублей0012-05-2025

Классификация: Экономика. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 18.48. Источник: www.mwananchi.co.tz.