Upasuaji huo umetumia saa tatu huku ukifanikiwa kutenganisha pacha walioungana aina ya walioungana (Parasitic conjoined twins).
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya upasuaji wa kutenganisha pacha walioungana aina ya (Parasitic conjoined twins).
Kwa mujibu wa MNH, hali ambayo ni nadra kutokea ambapo mmoja wa pacha hao hakui kikamilifu na humtegemea mwenzake kwa ukuaji na uhai.
Upasuaji huo umefanywa kwa mafanikio na madaktari wazawa wa MNH na hivyo kuandika historia nyingine muhimu katika sekta ya afya nchini, ambapo baada ya upasuaji mtoto anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari na wataalamu wa afya.
Akielezea ilivyokuwa leo Jumatatu, Agosti 10, 2026, Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto MNH, Victor Ngotta amesema upasuaji umekwenda vizuri na wamefanikiwa kupata mtoto huyo atakayeishi kawaida.
“Alikuwa ameungana sehemu yake ya ini, mtoto huyu aliyekamilika yeye ndiyo alikuwa anatoa damu kumpa huyo Parasitic twins ambaye hana viungo muhimu vya kumuwezesha kusafirisha damu kwenye mwili wake,” amefafanua.
Akifafanua maana ya aina hiyo ya pacha (Parasitic twins) Dk Ngotta anasema ni aina ya watoto walioungana ambapo mmoja anakuwa hajakamilika viungo vyote vinavyomfanya aishi.
“Katika upasuaji mkubwa wa leo tumeshirikisha na madaktari mabingwa ikiwemo wa usingizi na umekwenda vizuri kwa kufanikiwa kutenganisha,” amebainisha.
Amesema hospitali ya Muhimbili imeshatenganisha pacha walioungana ila aina hii ya (Parasitic conjoined twins) ndiyo mara ya kwanza kutenganishwa.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | EAC yageukia AI kukabili Ebola | 0 | 9.78 | 12-08-2026 |
| 2 | Mafanikio darasani yanaanzia kwenye afya ya mwili | 0 | 7.83 | 10-08-2026 |
| 3 | Mahitaji ya huduma za moyo Comoro yaipa fursa JKCI | 0 | 5.4 | 12-08-2026 |
| 4 | Sababu Tanzania kutunga sera mpya ya sayansi, teknolojia na ubunifu | 0 | 7.3 | 10-08-2026 |
| 5 | Usalama wa kihisia msingi muhimu utekelezaji wa mtalaa | 0 | 5.56 | 10-08-2026 |
| 6 | Twice-daily fumigation to curb spread of West Nile mosquito on Costa Tropical | 0 | 18.33 | 30-07-2026 |
| 7 | Разработан способ уничтожения раковых клеток вибрацией | 0 | 6.4 | 04-08-2026 |
| 8 | Паразит прогрыз глаз женщине после умывания | -2 | 7 | 15-07-2026 |
| 9 | Женщина прожила десять лет с 38 паразитами в мозге | -1 | 5 | 04-07-2026 |