Wanafunzi Watanzania wanaotamani kujikita katika teknolojia za kisasa wamepata fursa ya kusoma bila malipo sayansi ya data na Akili Unde (AI) katika Chuo Kikuu cha Tokyo, Japan, kwa miezi mitatu bure.
Dar es Salaam. Wanafunzi Watanzania wanaotamani kujikita katika teknolojia za kisasa wamepata fursa ya kusoma bila malipo sayansi ya data na Akili Unde (AI) katika Chuo Kikuu cha Tokyo, Japan, kwa miezi mitatu bure.
Fursa hiyo imetangazwa leo Jumatano, Agosti 12, 2026 na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, ukiwaalika wanafunzi kuomba nafasi ya mafunzo hayo yatakayotolewa kupitia Maabara ya Matsuo-Iwasawa ya Chuo Kikuu cha Tokyo.
Kwa mujibu wa tangazo hilo la ubalozi, mafunzo hayo yataanza Septemba 17 hadi Desemba 17, 2026, yakilenga kuwajengea washiriki ujuzi unaohitajika katika teknolojia zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa katika uchumi na soko la ajira la sasa na baadaye.
Kupitia tangazo hilo ubalozi umewataka wanafunzi wenye sifa nchini Tanzania kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi wao katika maeneo ya sayansi ya data na AI, ambayo yanaendelea kuwa muhimu katika maendeleo ya teknolojia na biashara duniani.
Miongoni mwa mada zitakazofundishwa ni sayansi ya data, ujifunzaji wa mashine, uchakataji na uwasilishaji wa data pamoja na matumizi ya sayansi ya data katika biashara.
Fursa hiyo inawalenga wanafunzi kuanzia ngazi ya sekondari hadi shahada ya uzamivu, huku waombaji wakitakiwa kuwa wanaosoma katika taasisi za elimu inayotambuliwa.
Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa mwanafunzi wakati wa kuanza kwa programu hiyo, awe na uwezo wa kujifunza kwa kujitegemea na kuwa tayari kushiriki kikamilifu katika mafunzo na kukamilisha mahitaji yake.
Kwa Tanzania, fursa hiyo inaweza kuwa sehemu ya kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi katika maeneo ya teknolojia yanayokua kwa kasi, hasa katika kipindi ambacho matumizi ya AI na uchanganuzi wa data yanaingia katika sekta mbalimbali za uchumi.
Tangazo hilo limewataka wanafunzi wanaotaka kuomba kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa Omnicampus, huku wakitakiwa kuwa na anuani ya barua pepe inayotumika.
“Baada ya usajili na kuidhinishwa, waombaji watapata taarifa za kuingia kwenye mfumo wa Omnicampus na kuendelea na hatua za maombi. Katika mfumo huo, mwombaji anatakiwa kuchagua kozi yenye jina “GCI World 2026 September” na kukamilisha maombi,” imeeleza taarifa hiyo.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Accordo Ue-Giappone su intelligenza artificiale e dati per servizi “senza barriere” | 0 | 9.07 | 05-05-2026 |
| 2 | Τελευταία εβδομάδα για αιτήσεις στο πρόγραμμα υποτροφιών AKTOR4TheFuture | 0 | 5 | 15-06-2026 |
| 3 | EAC yageukia AI kukabili Ebola | 0 | 9.78 | 12-08-2026 |
| 4 | Tusiache kuwalea hata kama wako vyuoni | 0 | 5 | 30-06-2026 |
| 5 | Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri | 0 | 10 | 12-08-2026 |
| 6 | Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo | 0 | 10 | 10-08-2026 |
| 7 | Осенью в 100 вузах России стартуют программы обучения технологиям ИИ | 0 | 0 | 22-07-2019 |
| 8 | Фан-та-сти-ка🔊 Запускаем Всероссийскую олимпиаду по искусственному интеллекту и раскрываем тему ... | 5 | 7 | 03-07-2026 |
| 9 | МТС, МФТИ и СКОЛКОВО набирают студентов в магистратуру "Цифровые технологии в бизнесе" | 0 | 0 | 02-07-2021 |
| 10 | Искусственный интеллект поможет в поиске работы выпускникам томского вуза | 0 | 0 | 23-11-2020 |